Thursday, 25 May 2017

DIAMOND AANDIKA HAYA JUU YA KIFO CHA IVAN

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mkali wa muziki Tanzania na Baba watoto wa Zari,Diamond Platinum ameandika maneno haya,'Mbele yako,Nyuma yetu', kufuatia kifo cha Ivan ambaye pia ni Baba watoto wa Zari.
Na:Esko Donald.

MZAZI MWENZAKE NA ZARI AFARIKI DUNIA.

Aliyekuwa mzazi mwenzake na Zari the boss Lady Ivan Ssemwanga amefariki dunia alipokuwa amelazwa Hospitalini nchini Afrika Kusini kutokana na matatizo ya moyo.Ivan alifanikiwa kupata watoto wa tatu na Zari.Taarifa zaidi nitakujuza.
Esko Madia Team tungependa kutoa pole juu ya msiba huu.R.I.P Ivan
Na:Esko Donald.

Wednesday, 24 May 2017

POUND 100,000 KWENDA KWA WAHANGA WA BOMU,MANCHESTER.

Kiungo wa Man City na raia wa Ivory Coast Yaya Toure na wakala wake D. Seluk wametoa Pound 100,000 ambazo ni zaidi ya Tsh.Millioni 200 kwa wahanga wa bomu huko jijini Manchester.Mlipuko huo ulitokea siku chache zilizopita.
Na:Esko Donald.

Tuesday, 23 May 2017

SILAHA MPYA NDANI YA WCB.

Naaaam,kwa mara nyingine WCB imekuletea msanii mpya kwenye lebo hiyo afahamikaye kwa jina la Lava Lava ambaye amekuja na ngoma yake mpya hiitwayo TUACHANE.Unaweza kuipata nyimbo hii kupitia tovuti ya Wasafi.com.
Wapenda mziki mzuri hakika wanategemea makubwa kutoka kwa msanii huyu.
Na:Esko Donald.

Sunday, 21 May 2017

BEN POL AFUNGUKA KUHUSU PICHA YAKE YA UTUPU KUZAGAA MTANDAONI

Mkali wa RNB nchini Ben Pol baada ya picha yake ya utupu kuzagaa mtandaoni,watu wengi wameonekana kulizungumzia hili suala kwa sura tofauti.Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ben Pol amefunguka na kuandika "Usi_judge kitabu kama haujakisoma".
Inasemekana kuna ujio mpya kutoka kwa Msanii huyu,ni nyimbo ijulikanayo kwa jina la "Mateka" na ndani ya nyimbo hiyo ameshirikishwa msanii Darassa.
Na:Esko Donald.

Wednesday, 17 May 2017

DOGO MFAUME AKUTWA NA UMAUTI.

Mkali wa Bongo flavour aliyewahi kutamba na nyimbo yake 'Kazi ya Dukani',amefariki leo katika hospitali ya Muhimbili.Mmiliki wa Sobber House alikokuwa akisaidiwa ili kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya amesema,Dogo Mfaume alikuwa afanyiwe upasuaji Ijumaa kutokana na uvimbe kwenye ubongo na alikuwa tayari ameshapangwa kwenye ratiba.
Ameongeza na kusema kuwa,Afya yake ilikuwa nzuri kabisa na alikuwa ana mwaka mmoja tangu ameacha matumizi ya dawa za kulevya 'UNGA' na walikuwa tayari wamejiandaa kwenda kumtolea damu.
R.I.P Dogo Mfaume.
Na:Esko Donald.

Monday, 15 May 2017

EBOLA KWA MARA NYINGINE,SASA NI DRC.

Shirika la Afya Duniani(WHO) limetangaza kuwa ugonjwa wa Ebola umezuka katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kusemekana kuwa kuna vifo vya watu watatu waliohusishwa kufa kwa ugonjwa huo.Shirika hilo limeanza kuchukua hatua dhidi ya ugonjwa huo.
Na:Esko Donald.

Sunday, 14 May 2017

WAFANYIWA MAOMBI AIR PORT,KIA.

Majeruhi wa ajali ya basi Arusha,Karatu wafanyiwa maombi wakiwa katika uwanja wa ndege wa KIA wakiwa katika hatua za awali kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya matibabu.
Na:Esko Donald.

MISHIPA YAKE ILIZIBULIWA KWA UTASHI

Ilikuwa ni Novemba 2011 katika kitengo cha tiba ya figo Muhimbili tulishuhudia mtoto Ali aliyekuwa na umri wa miaka 13 kutoka Rufiji mkoani Pwani akifanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu.Zoezi hili liliendeshwa na madaktari wa kitengo cha tiba ya figo Muhimbili wakishirikiana na madaktari kutoka India.
Na:Esko Donald.

ULIKUWA UNAMJUA HUYU.

Wengi tunafahamu kuwa kwa sasa WCB imekuwa ni Kampuni kubwa na yenye kutoa ajira kwa vijana wa Kitanzania.Na kama tunavyojua Kampuni yeyote ile huwa na wafanyakazi mbalimbali katika nafasi tofauti.
Kwa kulifahamu hilo leo nimeamua kukuletea mmoja kati ya wafanyakazi waliopo WCB,huyu ni Executive Secretary wa WCB anaitwa Lydia_Brown_bonphil.

Tuesday, 9 May 2017

JIFUNZE KUPITIA HADITHI FUPI.

HADITHI:LONICA.
MTUNZI:ESKO DONALD.
Esko Wa Simulizi 'EWS'
Whatsapp:0675730796
Ilikuwa ni siku ya Christmas December 25,msichana aliyefahamika kwa jina la Lonica anapitia kwenye Mgahawa kupata chakula cha mchana.Ilikuwa yapata saa nane na nusu mchana.Akiwa anaendelea na chakula ghafla kwenye meza aliyokuwa ameketi Lonica kunakuja kijana mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la Godwin.Wakiwa wanaendelea na maongezi Godwin aliamua kuomba number ya simu.Lonica bila kusita akatoa number.
Baada ya siku mbili kupita Godwin alianza kumtongoza Lonica na kudai kuwa alikuwa akimpenda sana.Ombi la Godwin kwa Lonica lilikuwa ni gumu sana kukubalika.Lonica hakutaka kuwa na Godwin kwenye mahusiano japokuwa kwa muda huo Lonica hakuwa na mtu kwenye mahusiano.Godwin hakutaka kukata tamaa,aliendelea kumsumbua Lonica ili aweze kumpata.Ilipita kama miezi nane mpaka Lonica alipokubali kuwa na Godwin kwenye mahusiano.Japokuwa Lonica hakumpenda Godwin ila kwa ushawishi wa Godwin ulimfanya Lonica aingie line mwenyewe.Safari ya mahusiano kati ya Godwin na Lonica ikaanza kwa matumaini huku kila mmoja akifurahia mahusiano yao.Ulipita mwaka mmoja tangu waanzishe mahusiano yao.
Kwa wakati huo wote walikuwa wakiishi jijini Mwanza.Lonica alikuwa akiishi kwa shangazi yake huku Godwin akiwa kwenye Chuo Kikuu cha SAUT kama mwanafunzi wa Ualimu kwa ngazi ya Shahada.
Lonica anapigiwa simu arudi kwa wazazi wake waliopo mkoani Arusha kwa lengo la kwenda kufanya kazi ya Stationary.Bila kupoteza muda Lonica anarudi mkoani Arusha alipozaliwa ambapo ndipo wazazi wake walipo.Baada ya wiki akiwa mkoani Arusha anaanza rasmi kazi kwenye Stationary iliyokuwa inamilikiwa na mjomba wake.Siku moja akiwa anaendelea na kazi,ghafla anatokea kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Ansell ambaye alikuja pale kwa lengo la kutoa Copy kitambulisho chake cha kupigia kura.Kwa hali isiyokuwa ya kawaida macho ya Ansell yalianza kuyashangaa macho ya Lonica huku macho ya Lonica nayo yakiyashangaa macho ya Ansell.Ni wazi wawili hawa walipendana kupindukia,kupitia ishara ya macho.
Ansell alipenda kutembelea pale Stationary mara kwa mara.Bila kupoteza wakati Ansell aliamua kumueleza ukweli mrembo Lonica kuwa alikuwa akimpenda sana.Kwa kuwa Lonica na yeye alikuwa akimpenda Ansell tangu siku ya kwanza,aliamua kukubali tena akiwa ni mwenye tabasamu maridhawa.Kwa wakati huu Godwin alikuwa bado yupo chuoni mkoani Mwanza.
Lonica alijikuta akiwa na mahusiano ya kimapenzi na wavulana wawili,yaani Ansell kijana mwenye mvuto pamoja na Godwin kijana msomi.Siku zilivyozidi kusonga Lonica alianza kuwa na mawazo ambayo yalisababishwa na yeye kuwa na mahusiano na wavulana wawili.Hakujua awe na yupi na amuache yupi.Baada ya miezi kadhaa Godwin alifanikiwa kumaliza chuo na kupata kazi huko huko mkoani Mwanza akiwa kama mwalimu wa Secondary.
Lonica baada ya kuwa na mawazo mengi aliamua kumuacha Ansell na kubaki na Godwin.
Ansell alikuwa akimpenda sana Lonica.Hata hivyo Lonica alikuwa akimpenda sana Ansell ila aliamua kuchukua maamuzi kama hayo.Lonica aliamua kwenda jijini Mwanza Kwa lengo la kumfuata Godwin.Kwa wakati huo Godwin alikuwa amepangangisha nyumba nzima.
Maamuzi aliyochukua Lonica yalimuhathiri Ansell Kisaikolojia.Aliumia sana.Muda wote alionekana kulia sana kama mtoto mchanga.Ansell alikuwa ni kibarua kwenye kiwanda cha mafuta ya kupikia.Hali ya mawazo ya muda wote ilimfanya ashindwe kwenda kazini.Bosi wa kiwanda hicho aliamua kumfukuza kazi Ansell.Kichwa kilikuwa kikimuuma kila wakati.
Upande wa Shilingi,Lonica aliendelea kufurahia maisha akiwa na Godwin huku Ansell akionekana kama chizi asiyejitambua.Mirindimo na mkusanyiko wa mawazo nafsini mwa Ansell ilisababisha moyo wake kuwa mkubwa hali ambayo ilipelekea apate presha mara kwa mara.Mara kwa mara alikuwa akipoteza fahamu.Mwili wa Ansell ulikonda sana.Hali ya huzuni kwa Ansell ilipelekea akose hamu ya kula.Aliweza kupitisha siku tatu bila kula chochote.Hali ya kukosa mlo kwa muda mredu ilipelekea Utumbo wa Ansell kujikunja.Maumivu makali ya tumbo yalisababisha akimbizwe Hospital kwa haraka kwa lengo la kuokoa maisha yake.Jitihada za majirani za kumpeleka Hospital haraka,hazikuweza kuzaa matunda kwa sababu kijana Ansell alifia njiani.
Madaktari walifanya uchunguzi kwa lengo la kubaini chanzo cha kifo chake.Baada ya uchunguzi kukamilika,inafahamika kuwa sehemu ya utumbo iliyojikunja ilikuwa imeoza vibaya na ingekuwa ngumu kupona.Mwili wa Ansell unazikwa kwa huzuni kubwa,huku kila mmoja akikumbuka ucheshi wake,ukarimu wake pamoja na kipaji chake cha uimbaji.Taarifa ya msiba inafika kwa Lonica lakini cha ajabu hakuonyesha Hali ya kushtuka wala kuguswa na msiba huo.Aliendelea kula bata na Godwin.
Mwili wa Ansell ulihifadhiwa salama chini ya ardhi.
Nyumbani kwa Godwin alikuwa akiishi Lonica,dada yake na Lonica aliyefahamika kwa jina la Marihana pamoja na Godwin mwenyewe.Kwa hali ya kushangaza Lonica anamkuta Godwin akiwa anafanya mapenzi na Marihana ambaye ndiye dada yake na Lonica.Godwin aliamua kuwachanganya wote wawili bila kujali chochote.Ugomvi mkubwa unatokea.Lonica anaamua kuondoka na kurudi jijini Arusha.
Lonica anaamua kwenda kulitazama kaburi la Ansell huku akibubujikwa na machozi mithili ya mvua za elnino.Alijikuta akisema maneno haya,huku akiwa amelala juu ya kaburi la Ansell,
"Ansell mpenzi nilishindwa kuchagua chaguo sahihi.Naomba unisamehe kwa kutokujali taarifa za msiba wako.Machozi yangu juu ya kaburi lako ni ishara ya kutaka msamaha wako.Naukumbuka sana upendo wako kwangu,ni kweli ulinipenda sana Ansell.Nakumbuka ulipokuwa unakuja nyumbani.Nakumbuka ulivyokuwa unafurahia kula chakula changu huku ukinisifia kuwa mimi ni mpishi bora kwako.Nakumbuka ulivyokuwa unapenda kuniita Mtu special na mimi nilikujibu kwa kukuita Special one.Naikumbuka kauli yako uliyokuwa unapendaga kusema,ulipenda kuniambia time will tell how much you love me.Nalikumbuka sana busu lako.Naikumbuka sana siku ya mwisho ambayo nili kiss na wewe.Naomba unisamehe Ansell,naomba Msamaha wako".
                     ......MWISHO......
        

Monday, 8 May 2017

KIPYA KUTOKA TV 1

Kituo cha televisheni cha TV 1 kinakuletea kipindi kipya kiitwacho Life & Style ambacho kitaanza kurushwa Jumanne saa tatu kamili usiku kikiongozwa na Mimi Mars.Usikose.
Na:Esko Donald.

MADEE AGUSWA NA KILIO CHA MZAZI,ARUSHA.

Hiki ndicho alichokiandika msanii Madee kwenye ukurasa wake kwa Twitter baada ya kuguswa na kilio cha mzazi aliyempoteza mtoto wake kwenye ajali iliyoua wanafunzi 32,Arusha.
Na:Esko Donald.

UMATI WAFURIKA KUAGA MIILI YA MAREHEMU,ARUSHA.

Huzuni yatanda kwenye viwanja vya Sheikh Abeid Arusha huku umati wa watu ukifurika viwanjani hapo kwa lengo la kuaga miili ya wanafunzi waliofariki kwa ajali ya gari,May 6,2017.
Na:Esko Donald.

IFAHAMU SIMU YENYE GHARAMA ZAIDI,2017.

Dunia ya sasa hivi imewekwa mkononi na teknolojia hususani kwenye matumizi ya simu.Asilimia kubwa ya watu hutumia simu za mikononi kwa ajili ya mawasiliano.
Leo nimekuletea simu yenye gharama zaidi kuliko zote duniani kwa mwaka huu ambayo imetengenezwa na kampuni la Apple.Simu hii inaitwa Diamond Rose iPhone 4 32GB yenye gharama ya Dola za Kimarekani million 8.Thamani ya simu hii inashika chati kutokana na simu hii kutengenezwa kwa material ya Almasi yenye thamani ya juu.

WASIFU WAKE,

Weight   140g(4.94 02)
Memory  32 GB,512 RAM
Display   3.5 inches
Camera  8 MP Back,Front 2 MP
Software IOS 4.0

Na:Esko Donald.

FATE 8 YAWASHA MOTO.

The Fate of the Furious ni movie iliyoandikwa na Chris Morgan huku bajeti yake ikikadiriwa kufikia dola million 250.Movie hii imeingizwa rasmi sokoni mnamo April 4,2017.Ukizungumzia movie inayofanya vizuri kwa sasa uwezi kuacha kuitaja The Fate of the furious(Au kwa jina jingine unaweza kuiita Fast and Furious 8 na Fast 8).
Kama bado haujapata nafasi ya kuitazama movie hii,ni wakati wa kufanya hivyo.Taarifa nyingine zinadai kuwa Fast and Furious 9 itatoka April 19,2019.
Na:Esko Donald.

Sunday, 7 May 2017

BREAKING NEWS:DAMU YAMWAGIKA MKOANI TANGA.

Mkoani Tanga,katika wilaya ya Muheza,Lusanga,kumetokea ajali mbaya iliyohusisha basi aina ya Coaster likitokea Tanga kuelekea Wilayani Korogwe limegonga Lori kwa nyuma na kusababisha vifo.Taarifa za awali zinasema watu wanne wamefariki hapo hapo ila waokoaji bado walikuwa wanaendelea na zoezi la uokoaji hivyo kuna uwezekano wa vifo kuongezeka.Maafa haya yametokea usiku huu.Taarifa zaidi nitakujuza.
Na:Esko Donald.

JIFUNZE KUPITIA HADITHI FUPI.


HADITHI:MWISHO WA NAFSI SALITI.
MTUNZI:ESKO DONALD.
Evans kijana mwenye ulemavu wa ngozi(Albino),akiwa kwenye chumba cha upasuaji anatolewa figo yake ya kulia na kubakiwa na ya kushoto kwa lengo la kumpatia rafiki yake kipenzi aitwaye Edgar ili kuyaokoa maisha yake.Figo ya Evans ilihitajika mwilini mwa Edgar ili aweze kuishi kwa sababu figo yake ya kulia ilikwisha athiriwa na sumu zilizojaa mwilini mwake.Urafiki wa Evans kijana mwenye ulemavu wa ngozi na Edgar kijana mwenye rangi nyeusi ulikuwa ni wa aina yake.Urafiki Wao ulikuwa ni wa kuigwa katika jamii.
Zoezi zima la upasuaji linakamilika.Evans anabaki na figo moja huku Edgar akipeta na figo mbili.Kadri siku zilivyozidi kusonga afya ya Edgar ilizidi kutengemaa.Taswira ya upendo uliokuwepo katikati yao uliweza kuimarisha hisia za kirafiki miongoni mwa watu wengi.Evans hakutamani kuona chozi la Edgar likidondoka bure wakati yeye angeliweza kuzuia uwepo wa majonzi moyoni mwa Edgar.Evans hakuwai kutoa maneno machafu wala kuihudhi nafsi ya Edgar nafsi ya Edgar na kumfanya akose raha.Edgar alikuwa ni kijana mwenye umri wa miaka ishirini na nane huku Evans akiwa ni kijana mwenye umri wa miaka ishirini na sita.Kipato chao kilipatikana kwa kuuza magodoro.
Baada ya miezi sita kupita,Edgar alisafiri na kwenda mkoa wa jirani.Kuanzia hapo biashara za Edgar azikuweza kufahamika na mtu yoyote yule kwani hata Evans hakuweza kutambua Edgar alijishughulisha na shughuli gani kwa kipindi hicho.
Ilikuwa ni mishale ya saa tisa za usiku baada ya Evans kuvamiwa na watu asiowajua chumbani mwake.Nyuso zao akuweza kuzitambua kwani zilifunikwa kwa vitambaa veusi usoni.Nyumba waliokuwa wakiishi Evans na Edgar haikuwa na uzio(fance),na vile vile chumba walichokipangisha mlango wake ulitazamia barabara kuu ya kuelekea mjini,hivyo ilikuwa ni rahisi kwa watu hawa kumvamia Evans.Kwa wakati huo ilisemekana Edgar alikuwa amesafiri miezi mitatu iliyopita.Viganja vya watu hao vilionekana kushikilia Mapanga yaliyong'aa kwa makali pamoja na misumemo ya kukatia mbao huku wangine wakiwa wameshikilia Masururu.
Ghafla ilisikika sauti kama ya Edgar ikisema,
"Oya mzibe mdomo tufanye kazi tusepe,biashara asubuhi bwana".
Kwa hali isiyokuwa ya kawaida waliivamia miguu ya Evans na kuanza kuikata maeneo ya kwenye magoti.Mapanga na misumemo ndio nyenzo walizotumia.
Ikasikika sauti kwa mara nyingine ikisema,
"Oya Edgar ebu shika msumeno vizuri acha kumuonea huruma,hizo ni pesa unazokata hapo"
Edgar akajibu,
"Poa Man ngoja nifanye fasta".
Kumbe Edgar rafiki kipenzi wa Evans kwa tamaa ya pesa na kuamini imani za kishirikina anaamua kumfanyia ukatili rafiki yake kipenzi.Aliamini kwa kukata miguu ya Evans angeweza kupata utajiri.Kwa kuwa Evans alikuwa amezibwa mdomo,sauti yake haikuweza kusikika isipokuwa macho yake yaliyojaa machozi yalikuwa yakitazama mikono ya Edgar ikatavyo miguu yake.Ukatili wao unakamilika na wanaamua kuondoka kwa haraka.Maumivu makali yasiyokuwa na ganzi yalirindima mwilini mwa Evans.Damu nyingi zilikuwa zikimtoka mwilini mwake.Nafsi ya Evans ilianza kuhisi harufu ya umauti ikimsogelea.Nafsi yake iliumia sana alipokumbuka maisha ya nyuma aliyoishi yeye pamoja na Edgar na tukio alilofanyiwa.Hatimaye Evans anakata roho huku Lita za damu zikiwa zimetapakaa sakafuni.
Gari dogo aina ya Verosa walilokuwa wamepanda Edgar na wenzake watatu lilikuwa likiendeshwa kwa kasi sana kuelekea nchi ya jirani.
Ghafla gurudumu la mbele upande wa kushoto likapasuka,
"PAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA\AAAAAAAAAAAAAAAAA".
Hali hii ilipelekea gari yao kuacha njia njia na kudondokea mabondeni.Baada ya ajali hiyo maiti moja iliyoharibika vibaya baada ya kupasuka vibaya maeneo ya kichwani ilipatikana pamoja na majeruhi watatu.Kumbe maiti hiyo ilikuwa ni mwili wa Edgar.Na huo ndio ulikuwa mwisho wa Edgar duniani.
Polisi wanafanya uchunguzi na kuikuta miguu ya Evans ikiwa imebanwa ndani ya boneti la gari iliyopata ajali.Polisi wanabaini kuwa watu hawa hawakuwa watu wema.Ulinzi mkali unawekwa kwa majeruhi watatu ambao walikuwa ni wenzake na Edgar.
Baada ya kupata nafuu,wanafunguliwa kesi ya mauaji na kuhukumiwa kunyongwa.
.............................................MWISHO...............................

Saturday, 6 May 2017

ATOKA BILA MAJERAHA HATA KIDOGO KWENYE AJALI ARUSHA.

Huyu ndiye mtoto aliyepona na kutoka bila hata jeraha kwenye ajali ya basi Arusha.

RAIS ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh.John Pombe Magufuli ameipokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya vifo vya wanafunzi 32,wakiwemo walimu wawili na dereva.Ametuma salamu za rambi rambi kuonyesha kuguswa na hili.
Ajali hii ilitokea baada ya basi walilopanda wanafunza hawa kuacha njia na kuangukia kwenye Korongo,Karatu mkoani Arusha walipokuwa wanaenda kufanya mtihani wa ujirani mwema kwenye shule inayofahamika kwa jina la Tumaini.
Wanafunzi hawa wa darasa la saba waliopata ajali ni wanafunzi kutoka shule ya msingi ya Lucky Vicent.
Na:Esko Donald.

KABLA YA UMAUTI.

Hii ndio picha ya Wanafunzi waliofariki Leo kwenye ajali ya gari jijini Arusha.
Hapa ni kabla ya Safari kuanza.
Na:Esko Donald.

DIAMOND KULITEKA SOKO.

Msanii wa kizazi kipya 'Diamond Platinum' ameingia kwenye mining'ono ya vinywa vya Watanzania wengi kutokana na kuja na bidhaa yake ya perfume ijulikanayo kwa jina la "CHIBU PERFUME".Amesema ilimchukia takribani miaka miwili kufanikisha hili.Aliongeza na kusema kuwa bidhaa yake ina ubora wa hali ya juu ukilinganisha na perfume zingine.Bidhaa hiyo ambayo imetengenezwa nchini Dubai inauzwa Sh.105000.Kwa mujibu wa yeye mwenyewe alisema bei hii imezingatia na ubora wa bidhaa yenyewe.
Kwa sasa CHIBU PERFUME inafanya vizuri sokoni tofauti na mategemeo ya wengi.
Na:Esko Donald.

POLISI ARUSHA WATHIBITISHA NI ZAIDI YA WATU 30 WALIOFARIKI KWENYE AJALI LEO.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema idadi ya waliofariki ni 32 akiwemo dereva kwenye kundi la watu wazima watatu,wavulana ni 12 na wasichana ni 17.Ajali hii imetokea Leo May 6,2017 kwenye eneo la Mlima Rhotia,Karatu mkoani Arusha.
Imeripotiwa kuwa ajali hii ilihusisha basi la wanafunzi ambao walikuwa wanakwenda kufanya mtihani wa ujirani mwema.
Inasemekana dereva wa basi hilo aliyejulikana kwa jina la Luck Vicent alishindwa kuliongoza vizuri basi hilo wakati akikata kona kwenye mteremko hivyo lilimshinda na kuingia kwenye korongo na kusababisha umauti wa roho 32.
Na:Esko Donald.

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...