Tuesday, 9 May 2017

JIFUNZE KUPITIA HADITHI FUPI.

HADITHI:LONICA.
MTUNZI:ESKO DONALD.
Esko Wa Simulizi 'EWS'
Whatsapp:0675730796
Ilikuwa ni siku ya Christmas December 25,msichana aliyefahamika kwa jina la Lonica anapitia kwenye Mgahawa kupata chakula cha mchana.Ilikuwa yapata saa nane na nusu mchana.Akiwa anaendelea na chakula ghafla kwenye meza aliyokuwa ameketi Lonica kunakuja kijana mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la Godwin.Wakiwa wanaendelea na maongezi Godwin aliamua kuomba number ya simu.Lonica bila kusita akatoa number.
Baada ya siku mbili kupita Godwin alianza kumtongoza Lonica na kudai kuwa alikuwa akimpenda sana.Ombi la Godwin kwa Lonica lilikuwa ni gumu sana kukubalika.Lonica hakutaka kuwa na Godwin kwenye mahusiano japokuwa kwa muda huo Lonica hakuwa na mtu kwenye mahusiano.Godwin hakutaka kukata tamaa,aliendelea kumsumbua Lonica ili aweze kumpata.Ilipita kama miezi nane mpaka Lonica alipokubali kuwa na Godwin kwenye mahusiano.Japokuwa Lonica hakumpenda Godwin ila kwa ushawishi wa Godwin ulimfanya Lonica aingie line mwenyewe.Safari ya mahusiano kati ya Godwin na Lonica ikaanza kwa matumaini huku kila mmoja akifurahia mahusiano yao.Ulipita mwaka mmoja tangu waanzishe mahusiano yao.
Kwa wakati huo wote walikuwa wakiishi jijini Mwanza.Lonica alikuwa akiishi kwa shangazi yake huku Godwin akiwa kwenye Chuo Kikuu cha SAUT kama mwanafunzi wa Ualimu kwa ngazi ya Shahada.
Lonica anapigiwa simu arudi kwa wazazi wake waliopo mkoani Arusha kwa lengo la kwenda kufanya kazi ya Stationary.Bila kupoteza muda Lonica anarudi mkoani Arusha alipozaliwa ambapo ndipo wazazi wake walipo.Baada ya wiki akiwa mkoani Arusha anaanza rasmi kazi kwenye Stationary iliyokuwa inamilikiwa na mjomba wake.Siku moja akiwa anaendelea na kazi,ghafla anatokea kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Ansell ambaye alikuja pale kwa lengo la kutoa Copy kitambulisho chake cha kupigia kura.Kwa hali isiyokuwa ya kawaida macho ya Ansell yalianza kuyashangaa macho ya Lonica huku macho ya Lonica nayo yakiyashangaa macho ya Ansell.Ni wazi wawili hawa walipendana kupindukia,kupitia ishara ya macho.
Ansell alipenda kutembelea pale Stationary mara kwa mara.Bila kupoteza wakati Ansell aliamua kumueleza ukweli mrembo Lonica kuwa alikuwa akimpenda sana.Kwa kuwa Lonica na yeye alikuwa akimpenda Ansell tangu siku ya kwanza,aliamua kukubali tena akiwa ni mwenye tabasamu maridhawa.Kwa wakati huu Godwin alikuwa bado yupo chuoni mkoani Mwanza.
Lonica alijikuta akiwa na mahusiano ya kimapenzi na wavulana wawili,yaani Ansell kijana mwenye mvuto pamoja na Godwin kijana msomi.Siku zilivyozidi kusonga Lonica alianza kuwa na mawazo ambayo yalisababishwa na yeye kuwa na mahusiano na wavulana wawili.Hakujua awe na yupi na amuache yupi.Baada ya miezi kadhaa Godwin alifanikiwa kumaliza chuo na kupata kazi huko huko mkoani Mwanza akiwa kama mwalimu wa Secondary.
Lonica baada ya kuwa na mawazo mengi aliamua kumuacha Ansell na kubaki na Godwin.
Ansell alikuwa akimpenda sana Lonica.Hata hivyo Lonica alikuwa akimpenda sana Ansell ila aliamua kuchukua maamuzi kama hayo.Lonica aliamua kwenda jijini Mwanza Kwa lengo la kumfuata Godwin.Kwa wakati huo Godwin alikuwa amepangangisha nyumba nzima.
Maamuzi aliyochukua Lonica yalimuhathiri Ansell Kisaikolojia.Aliumia sana.Muda wote alionekana kulia sana kama mtoto mchanga.Ansell alikuwa ni kibarua kwenye kiwanda cha mafuta ya kupikia.Hali ya mawazo ya muda wote ilimfanya ashindwe kwenda kazini.Bosi wa kiwanda hicho aliamua kumfukuza kazi Ansell.Kichwa kilikuwa kikimuuma kila wakati.
Upande wa Shilingi,Lonica aliendelea kufurahia maisha akiwa na Godwin huku Ansell akionekana kama chizi asiyejitambua.Mirindimo na mkusanyiko wa mawazo nafsini mwa Ansell ilisababisha moyo wake kuwa mkubwa hali ambayo ilipelekea apate presha mara kwa mara.Mara kwa mara alikuwa akipoteza fahamu.Mwili wa Ansell ulikonda sana.Hali ya huzuni kwa Ansell ilipelekea akose hamu ya kula.Aliweza kupitisha siku tatu bila kula chochote.Hali ya kukosa mlo kwa muda mredu ilipelekea Utumbo wa Ansell kujikunja.Maumivu makali ya tumbo yalisababisha akimbizwe Hospital kwa haraka kwa lengo la kuokoa maisha yake.Jitihada za majirani za kumpeleka Hospital haraka,hazikuweza kuzaa matunda kwa sababu kijana Ansell alifia njiani.
Madaktari walifanya uchunguzi kwa lengo la kubaini chanzo cha kifo chake.Baada ya uchunguzi kukamilika,inafahamika kuwa sehemu ya utumbo iliyojikunja ilikuwa imeoza vibaya na ingekuwa ngumu kupona.Mwili wa Ansell unazikwa kwa huzuni kubwa,huku kila mmoja akikumbuka ucheshi wake,ukarimu wake pamoja na kipaji chake cha uimbaji.Taarifa ya msiba inafika kwa Lonica lakini cha ajabu hakuonyesha Hali ya kushtuka wala kuguswa na msiba huo.Aliendelea kula bata na Godwin.
Mwili wa Ansell ulihifadhiwa salama chini ya ardhi.
Nyumbani kwa Godwin alikuwa akiishi Lonica,dada yake na Lonica aliyefahamika kwa jina la Marihana pamoja na Godwin mwenyewe.Kwa hali ya kushangaza Lonica anamkuta Godwin akiwa anafanya mapenzi na Marihana ambaye ndiye dada yake na Lonica.Godwin aliamua kuwachanganya wote wawili bila kujali chochote.Ugomvi mkubwa unatokea.Lonica anaamua kuondoka na kurudi jijini Arusha.
Lonica anaamua kwenda kulitazama kaburi la Ansell huku akibubujikwa na machozi mithili ya mvua za elnino.Alijikuta akisema maneno haya,huku akiwa amelala juu ya kaburi la Ansell,
"Ansell mpenzi nilishindwa kuchagua chaguo sahihi.Naomba unisamehe kwa kutokujali taarifa za msiba wako.Machozi yangu juu ya kaburi lako ni ishara ya kutaka msamaha wako.Naukumbuka sana upendo wako kwangu,ni kweli ulinipenda sana Ansell.Nakumbuka ulipokuwa unakuja nyumbani.Nakumbuka ulivyokuwa unafurahia kula chakula changu huku ukinisifia kuwa mimi ni mpishi bora kwako.Nakumbuka ulivyokuwa unapenda kuniita Mtu special na mimi nilikujibu kwa kukuita Special one.Naikumbuka kauli yako uliyokuwa unapendaga kusema,ulipenda kuniambia time will tell how much you love me.Nalikumbuka sana busu lako.Naikumbuka sana siku ya mwisho ambayo nili kiss na wewe.Naomba unisamehe Ansell,naomba Msamaha wako".
                     ......MWISHO......
        

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...