Na:Esko Donald.
Esko Wa Simulizi 'EWS'.
Jesca binti wa Kimasai mwenye rangi ya bahati kuliko mabinti wote kijijini kwao alikuwa ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto watatu yani yeye Jesca na wadogo zake wawili,Oropi na Singoi.
Uzuri wa Jesca haukujificha machoni pa wengi,kila mmoja alipenda kumtazama muda wote.Ilifika wakati vijana walikuwa wakisema kumtazama Jesca kwa dakika tano basi kutakuongezea maisha marefu duniani.Alama yake ya kidoti chenye rangi nyeusi usoni mwake kilinogesha uzuri wake.Maisha yalikuwa niya furaha sana kwenye familia yao.
Jesca anapata bahati ya kufika chuo kikuu kuchukua degree yake ya kwanza.Wazazi wa Jesca japokuwa walikuwa na maisha ya kawaida ila walijitahidi kumsomesha mtoto wao mpaka chuo kikuu.Alikuwa anachukua shahada ya udaktari wa wanyama.Akiwa Mwaka wa mwisho kuelekea kwenye mitihani ya kumaliza elimu yake anapigiwa simu na kupewa taarifa ya kifo cha mama yake mzazi.Jesca anajikuta anapoteza fahamu kwa masaa nane asijitambue.Baada ya muda kupita Jesca anarejewa na ufahamu asijue la kufanya kwa wakati huo.
Katika hali ya mshangao kunapigwa simu kutoka kijijini kwa kina Jesca na kutoa taarifa nyingine nzito ambayo iliupasua moyo wa Jesca na kulegeza viungo vyake vyote vya mwili wake.Ilikuwa ni taarifa nyingine ya msiba.Simu ilitoa taarifa juu ya kifo cha baba yake Jesca pamoja na wadogo zake wawili,kwa sasa familia nzima ya Jesca ilipoteza maisha.Baada ya kifo cha mama yake ambaye alikuwa anasumbuliwa na kisukari,maandalizi ya mazishi yalianza huku watu wakiwa wanamsubiri Jesca kwa ajili ya mazishi.Mwili wa mama yake Jesca baada ya kutoka hospitali moja kwa moja uliletwa nyumbani kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.Ilikuwa ni majira ya usiku mwili wa mama Jesca ukiwa ndani huku pembezoni mwake ukiwa umezungurushiwa mishumaa,ghafla mshumaa mmoja unadondoka chini ambapo ulikutana na godoro ambalo walikuwa wamelalia baba yake Jesca na wadogo zake.Kwa hali isiyokuwa ya kawaida nyumba nzima inawaka moto.Moto huo uliteketeza kila kitu ikiwemo mwili wa aliyekuwa marehemu mama Jesca,baba Jesca na wadogo zake.Hakuna kitu kilichotoka salama.Chumba ambacho familia ya Jesca ilikuwa imelala ndicho chumba ambacho mwili wa mama Jesca ulikuwa umehifadhiwa ndio maana ilikuwa rahisi wote kupoteza maisha.
Jesca alilia mpaka sauti ikapotea,alitamani iwe ndoto kwa haya yaliyomkuta.Aliyakumbuka maisha ya furaha aliyoishi na familia yake.Alitamani familia yake ile matunda kutoka kwake kwani walipambana kumsomesha.Kibaya zaidi kinachompa simanzi ni kukosa kuiona miili ya wazazi wake pamoja na wadogo zake kwa sababu iliteketea kwa moto na kubaki majivu.
BAADA YA MIAKA MITATU.
Jesca anapokea simu na kuambiwa kifo cha wazazi wake pamoja na wadogo zake ni njama iliyofanywa na mtu wake wa karibu ambaye ni mpenzi wake,mvulana ambaye walipendana sana.Anaambiwa kuwa mpenzi wake ndiye amepelekea maafa haya kutokea.
ITAENDELEA……….
No comments:
Post a Comment