HADITHI:MWISHO WA NAFSI SALITI.
MTUNZI:ESKO DONALD.
Evans kijana mwenye ulemavu wa ngozi(Albino),akiwa kwenye chumba cha upasuaji anatolewa figo yake ya kulia na kubakiwa na ya kushoto kwa lengo la kumpatia rafiki yake kipenzi aitwaye Edgar ili kuyaokoa maisha yake.Figo ya Evans ilihitajika mwilini mwa Edgar ili aweze kuishi kwa sababu figo yake ya kulia ilikwisha athiriwa na sumu zilizojaa mwilini mwake.Urafiki wa Evans kijana mwenye ulemavu wa ngozi na Edgar kijana mwenye rangi nyeusi ulikuwa ni wa aina yake.Urafiki Wao ulikuwa ni wa kuigwa katika jamii.
Zoezi zima la upasuaji linakamilika.Evans anabaki na figo moja huku Edgar akipeta na figo mbili.Kadri siku zilivyozidi kusonga afya ya Edgar ilizidi kutengemaa.Taswira ya upendo uliokuwepo katikati yao uliweza kuimarisha hisia za kirafiki miongoni mwa watu wengi.Evans hakutamani kuona chozi la Edgar likidondoka bure wakati yeye angeliweza kuzuia uwepo wa majonzi moyoni mwa Edgar.Evans hakuwai kutoa maneno machafu wala kuihudhi nafsi ya Edgar nafsi ya Edgar na kumfanya akose raha.Edgar alikuwa ni kijana mwenye umri wa miaka ishirini na nane huku Evans akiwa ni kijana mwenye umri wa miaka ishirini na sita.Kipato chao kilipatikana kwa kuuza magodoro.
Baada ya miezi sita kupita,Edgar alisafiri na kwenda mkoa wa jirani.Kuanzia hapo biashara za Edgar azikuweza kufahamika na mtu yoyote yule kwani hata Evans hakuweza kutambua Edgar alijishughulisha na shughuli gani kwa kipindi hicho.
Ilikuwa ni mishale ya saa tisa za usiku baada ya Evans kuvamiwa na watu asiowajua chumbani mwake.Nyuso zao akuweza kuzitambua kwani zilifunikwa kwa vitambaa veusi usoni.Nyumba waliokuwa wakiishi Evans na Edgar haikuwa na uzio(fance),na vile vile chumba walichokipangisha mlango wake ulitazamia barabara kuu ya kuelekea mjini,hivyo ilikuwa ni rahisi kwa watu hawa kumvamia Evans.Kwa wakati huo ilisemekana Edgar alikuwa amesafiri miezi mitatu iliyopita.Viganja vya watu hao vilionekana kushikilia Mapanga yaliyong'aa kwa makali pamoja na misumemo ya kukatia mbao huku wangine wakiwa wameshikilia Masururu.
Ghafla ilisikika sauti kama ya Edgar ikisema,
"Oya mzibe mdomo tufanye kazi tusepe,biashara asubuhi bwana".
Kwa hali isiyokuwa ya kawaida waliivamia miguu ya Evans na kuanza kuikata maeneo ya kwenye magoti.Mapanga na misumemo ndio nyenzo walizotumia.
Ikasikika sauti kwa mara nyingine ikisema,
"Oya Edgar ebu shika msumeno vizuri acha kumuonea huruma,hizo ni pesa unazokata hapo"
Edgar akajibu,
"Poa Man ngoja nifanye fasta".
Kumbe Edgar rafiki kipenzi wa Evans kwa tamaa ya pesa na kuamini imani za kishirikina anaamua kumfanyia ukatili rafiki yake kipenzi.Aliamini kwa kukata miguu ya Evans angeweza kupata utajiri.Kwa kuwa Evans alikuwa amezibwa mdomo,sauti yake haikuweza kusikika isipokuwa macho yake yaliyojaa machozi yalikuwa yakitazama mikono ya Edgar ikatavyo miguu yake.Ukatili wao unakamilika na wanaamua kuondoka kwa haraka.Maumivu makali yasiyokuwa na ganzi yalirindima mwilini mwa Evans.Damu nyingi zilikuwa zikimtoka mwilini mwake.Nafsi ya Evans ilianza kuhisi harufu ya umauti ikimsogelea.Nafsi yake iliumia sana alipokumbuka maisha ya nyuma aliyoishi yeye pamoja na Edgar na tukio alilofanyiwa.Hatimaye Evans anakata roho huku Lita za damu zikiwa zimetapakaa sakafuni.
Gari dogo aina ya Verosa walilokuwa wamepanda Edgar na wenzake watatu lilikuwa likiendeshwa kwa kasi sana kuelekea nchi ya jirani.
Ghafla gurudumu la mbele upande wa kushoto likapasuka,
"PAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA\AAAAAAAAAAAAAAAAA".
Hali hii ilipelekea gari yao kuacha njia njia na kudondokea mabondeni.Baada ya ajali hiyo maiti moja iliyoharibika vibaya baada ya kupasuka vibaya maeneo ya kichwani ilipatikana pamoja na majeruhi watatu.Kumbe maiti hiyo ilikuwa ni mwili wa Edgar.Na huo ndio ulikuwa mwisho wa Edgar duniani.
Polisi wanafanya uchunguzi na kuikuta miguu ya Evans ikiwa imebanwa ndani ya boneti la gari iliyopata ajali.Polisi wanabaini kuwa watu hawa hawakuwa watu wema.Ulinzi mkali unawekwa kwa majeruhi watatu ambao walikuwa ni wenzake na Edgar.
Baada ya kupata nafuu,wanafunguliwa kesi ya mauaji na kuhukumiwa kunyongwa.
.............................................MWISHO...............................
Sunday, 7 May 2017
JIFUNZE KUPITIA HADITHI FUPI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
JIFUNZE KUPITIA HADITHI.
…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...

-
Linapojatwa jina la Director Nisher bila shaka itakuwa unakumbuka video ya nyimbo ya Young D "Kijukuu" na nyingine nyingi ambazo z...
-
Na:Esko Donald. Esko Wa Simulizi 'EWS'. Jesca binti wa Kimasai mwenye rangi ya bahati kuliko mabinti wote kijijini kwao alikuwa ni...
-
Madrid yafanikiwa kuandika historia mpya baada ya kulichukua kombe hili mara mbili mfululizo.
-
Bila shaka ni wengi hatumfahamu Lemma Guya Gemeda,huyu ni mchoraji maarafu kutoka nchini Ethiopia.Lemma ana umri wa miaka 90 na amechora zai...
-
……JESCA…… Episode ya 2 Na:Esko Donald. Esko Wa Simulizi 'EWS'. Whatsapp:0675730796. Ilipoishia.. BAADA YA MIAKA MITATU. Jesca...
Inasikitisha sana rafiki yako wa karibu unamtenda ubaya kisa Mali??? Hivi ndivyo ilivyo hata Leo mambo madogo yanatutenganisha na ndugu jamaa, na marafiki pia
ReplyDeleteAsante kwa maoni
Delete