Thursday, 31 August 2017

NYIMBO MPYA:DIAMOND X PATORANKING

Ile kolabo kali iliyowahusisha wakali wawili,yaani Diamond Platinum kutoka Tanzania na Patoranking kutoka Nigeria ni leo.Muda wowote kuanzia sasa nyimbo hiyo itakuwa hewani,kaa mkao kula shabiki mpenda mziki mzuri.
Na:Esko Donald.

Wednesday, 23 August 2017

NILIAMBIWA WABAYA WANGU NI RAFIKI ZANGU_ROMA

Msanii wa Hip Hop nchini,Roma Mkatoliki amesema kuwa baada ya kupata matatizo kuna maneno mengi alikuwa akiambiwa na watu mbalimbali ambayo yangeweza kumgombanisha na watu wake wa karibu.Aliyasema haya alipokuwa anahojiwa na Ayo TV na kusema kuwa yalizuka maneno ambayo yalidai kuwa waliohusika kusuka tukio zima la kutekwa kwake ni watu wake wa karibu,na kama angejaribu kuyaamini angegombana na rafiki Zake wa karibu.
Na:Esko Donald.

Friday, 18 August 2017

PEMBE ZA NDOVU ZAPATIKANA KWENYE MOJA YA GHALA MBEZI BEACH.

Hatimaye jeshi la Polisi jijini Dar es salaam limekamata pembe za Ndovu zipatazo 21 katika moja ya ghala lililopo maeneo ya Mbezi Beach jijini humo huku watu sita wakiwekwa mbaroni kwa tuhuma za kuhusishwa na pembe hizo.
Na:Esko Donald.

IDADI YA WALIOFARIKI SIERRA LEONE NI ZAIDI YA 400.

Umoja wa Mataifa UN umesema idadi ya watu waliofariki Nchini Sierra Leone baada ya kutokea Mafuriko katika Mji mkuu wa Nchini hiyo huitwao Freetown ni zaidi ya 400 huku wengine wakikadiriwa kufikia 600 hawajapatikana.
Na:Esko Donald.

WANAFUNZI 22 WAPANDISHWA KIZIMBANI.

Wanafunzi wapatao 22 wa ya Shule ya Sekondari Mirambo ya Tabora wamepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka 12 kwa kudaiwa kufanya uvamizi na kuwajeruhi watu 6.
Na:Esko Donald.

Thursday, 17 August 2017

UMATI WA WATU WAZIKWA,SIERRA LEONE.

Wizara ya afya nchini Sierra Leone imesema takriban nusu ya maiti 400 zitokanazo na maporomoko ya udongo na mafuriko nje ya mji wa Freetown tayari zimezikwa.
Serikali ilisema mazishi ya pamoja yangeahirishwa hadi leo ili kutoa fursa kwa ndugu na jamaa kutambua miili ya maiti ya waathirika.
Imefahamika kuwa mazishi hayo yamehusisha miili ambayo tayari ilitambuliwa au ilikuwa imeharibika kabisa.
Watu wapatao mia sita mpaka sasa bado hawajulikani walipo.
Rais wa Sierra Leone ametangaza siku saba za maombolezi.
Nathaniel Williams ni daktari katika hospitali kuu ya Connaught, iliyopo Freetown, anasema hivi sasa kuna tahadhari kubwa ya kutokea magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu.
Ameongeza kusema kuwa hivi sasa kunahitajika madawa na vyakula, kwa wale walioathirika.
Hata hivyo, Umoja wa Mataifa nchini humo umesema tayari umeweka mikakati ya kuweza kukabiliana na magonjwa ya milipuko iwapo yatatokea.
Source:bbcswahili.
Na:Esko Donald.

Tuesday, 15 August 2017

ODINGA KUWEKA MAMBO HADHARANI JUU YA WIZI WA KURA.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais uliopita ameliambia gazeti la Financial Times nchini Uingereza kwamba atafichua ushahidi siku ya
Jumanne kuhusu vile alivyoibiwa kura.

''Tutauonyesha ulimwengu ulivyochezewa''.

Bwana Odinga ambaye alikuwa akiwania urais kwa mara ya nne pia alibaini kwamba hatowania tena urais na kwamba aliwataka Wakenya kujua kilichofanyika wakati wa uchaguzi huo.
''Sio swala la kuwa mbifansi, Sio swala kuhusu Raila Odinga, Sitawania urais tena......tunataka Wakenya kujua kile kilichofanyika, na kile ambacho ulimwengu haujui kinafanyika''.
Bwana Odinga amedai kwamba wadukuzi waliingilia kompyuta za tume ya Uchaguzi na kuweka hesabu ambazo zilimpatia ushindi rais Uhuru Kenyatta.
Source:bbcswahili.
Na:Esko Donald.

Monday, 14 August 2017

ODINGA AWATAKA WAFUASI WAKE KUSUSIA KAZI SIKU YA LEO.

Kinara wa muungano upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amewashauri wafuasi wake kususia kazi siku ya Jumatatu kama njia ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumanne iliyopita.
Akihutubia wafuasi wake mtaani Kibera, Nairobi kwa mara ya kwanza kabisa tangu kutangazwa matokeo, ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi, Bw Odinga amedai kuwa serikali ilikuwa imepanga kuwaua wafuasi wa upinzani kabla ya kutangazwa matokeo.
Source:bbcswahili.
Na:Esko Donald.

Sunday, 13 August 2017

VURUGU ZAUWA WATU NCHINI KENYA.

Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya, ambao ulishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, umeapa kuendelea na maandamano wenye nia ya kubatilisha kile ambacho unasema kuwa, matokeo "feki" ya uchaguzi mkuu.
Mpinzani mkuu wa Bw Kenyatta, Bw Raila Odinga, amedai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na wizi mkubwa wa kura.
Upinzani Kenya wadai Odinga ndiye mshindi wa urais.
Seneta James Orengo ameiambia BBC kuwa chama chake, kinachoongozwa na Bw Raila Odinga, hakitapinga matokeo ya uchaguzi mkuu mahakamani, huku akisema kuwa Uhuru Kenyatta tayari ametoa vitisho kwa majaji.
Kufikia sasa watu 11 wameuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu, ambazo zilianza mara tu baada ya Uhuru Kenyatta kushinda kutangazwa mshindi kwa muhula wa pili mnamo usiku wa kuamkia Jumamosi.
Tume ya taifa ya kutetea haki za kibinadamu nchini Kenya, imetoa orodha ya juu ya wahasiriwa wa ghasia hizo huku ikisema kuwa ni watu 24 ndio ambao wameuwawa katika visa vinavyohusiwa na uchaguzi huo, huku ikiongeza kuwa polisi wanatumia nguvu kupita kiasi.
Kaimu Waziri wa usalama wa ndani, Fred Matiangi, amewataja waandamanaji kama "wahalifu".
Source:bbcswahili.
Na:Esko Donald.

Thursday, 10 August 2017

ODINGA AISHANGAZA TUME KWA KUJITANGAZIA MATOKEO.

Tume ya Uchaguzi ya Kenya imesema ni mapema na ni kinyume cha sheria kwa mgombea wa upinzani Raila Odinga kujitangazia kuwa ameshinda uchaguzi wa Kenya.
Alhamisi, muungano wa upinzani wa NASA ulichapisha matokeo ambayo yanaonyesha kuwa Raila Odinga amemshinda Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, ambapo pia waliitaka tume ya uchaguzi imtangaze Odinga kuwa ndiye Rais mteule.
Hata hivyo matokeo ya awali hadi sasa yaliyotangazwa na tume hiyo yanaonyesha Rais wa sasa Uhuru Kenyatta bado anaongoza dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga.
Source:bbcswahili
Na:Esko Donald.

BILL GATES AMIMINA MAPESA TANZANIA

Hii ni taarifa njema kwako Mtanzania. Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation imetenga Dola za Marekani 350 sawa na takribani shillingi Billioni 777.084 za Tanzania Kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika sekta ya Kilimo, afya na mifumo ya kielektroniki ya upatikanaji wa taarifa.
Na:Esko Donald.

UCHAGUZI KENYA.


Ni siku ya tatu sasa tangu Wakenya walipofika katika vituo vya kura kuwachagua viongozi na matokeo kamili ya uchaguzi wa urais yanaendelea kusubiriwa.
Na:Esko Donald.

Wednesday, 9 August 2017

TIGO YAZIDI KUTIMUA VUMBI.

Kampuni la mitandao ya simu la Tigo limezidi kutimua vumbi na kuwaacha wengi midomo wazi.Kwa kuonyesha linawajali wateja wake,sasa hivi wamekuja na App yao ambayo inaitwa Tigo App.App hii itamuwezesha mteja kununua bidhaa,kuangalia balance,utanunua data bundles na mengine mengi.Utaweza kuipata App hii kama una simu ya Android au IOS phone na pia unatakiwa kuwa na Line yako ya tigo iliyosajiliwa.
Pakua App hii ufurahie maisha.
Na:Esko Donald.

Tuesday, 8 August 2017

ODINGA AKATAA MATOKEO.

Mgombea urais wa muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) Raila Odinga amepinga matokeo ambayo yanaendelea kutangazwa na tume ya uchaguzi nchini humo, IEBC.
Bw Odinga amewaambia wanahabari kwamba tume hiyo imekuwa ikitangaza matokeo kwenye tovuti yake bila kufuata utaratibu ufaao.
Waziri mkuu huyo wa zamani amesema kabla ya matokeo yoyote kutangazwa, IEBC inafaa kuwapa maajenti wa vyama Fomu 34A kutoka vituoni.
Amesema kwa sasa, bila kuwepo kwa fomu hizo, ni vigumu kubaini matokeo yanayopeperushwa yanatoka wapi.
"Mfumo umeacha kufanya kazi. Sasa ni mitambo inayopiga kura. IEBC wamesema kwamba hakuna chama chochote kilichopinga matokeo. Lakini vyama vitapingaje matokeo bila kujua asili yake? Ni fomu 34A pekee zinazoonesha chanzo cha matokeo," amesema.
"Kwa hivyo, tunakataa matokeo yote yaliyotangazwa kwa sasa na kuitaka tume ya IEBC itoe fomu 34A za kila kituo kabla ya matokeo zaidi kutangazwa."
IEBC imekuwa ikitangaza matokeo ya urais mtandaoni, na kufikia saa tisa na robo alfajiri, matokeo hayo yalikuwa yanamuonyesha Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee akiwa mbele na kura 6331140 (55.27%) naye Bw Odinga akiwa na kura 5031737 (43.92%).
Matokeo hayo ni ya kutoka vituo 295319 kati ya vituo 40883 nchini humo.
"Hii ni kompyuta inayopiga kura," alisema Bw Odinga akikataa matokeo hayo.
Hali ya wasiwasi imekuwa ikitanda katika kituo cha taifa cha kujumlishia na kutangaza matokeo katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi.
Matokeo yalianza kutiririka baadaye Jumanne jioni baada ya shughuli ya kuhesabiwa kura kuanza. Matokeo hayo yamekuwa yakionesha Bw Kenyatta akiongoza.
Source:bbc Swahili.
Na:Esko Donald.

JIONEE MAAJABU KUTOKA TIGO.

Tigo wamekuletea simu nyingine yenye upekee wa aina yake.Hii ni TECNO Camon  CX 4G yenye kamera ya mbele 16MP na pia ina Memory yenye 16 GB,2 GB.
Ni kwa 399,900 TZS unapata hii simu.Haiishii hapo kwani kwa kununua simu hii kutoka Tigo utapata 1GB kwa ajili ya Internet kwa kila mwezi ndani ya miezi mitatu.
Na:Esko Donald.

FAHAMU MADHARA YA KULA NYAMA ISIYOIVA VIZURI AU MBICHI KABISA.


Kupitia video hii utaweza kufahamu madhara yatokanayo na kula nyama ambayo haija vizuri mbichi kabisa.
Na;Esko Donald

Wednesday, 2 August 2017

SHAMBULIZI LA FISI KIJIJINI BALANG'DALALU.

Mkulima mmoja mkoani Manyara katika Wilaya ya Hanang,kijiji cha Balang'dalalu avamiwa na fisi kwenye zizi lake la ng'ombe usiku wa kuamkia leo,mishale ya saa nane usiku.
Fisi huyo alifanikiwa kumjeruhi vibaya ng'ombe mmoja kwa kumng'ata maeneo ya mdomoni kuelekea eneo la juu ya uso.
Mkulima huyo alisema kuwa,alishtuka baada ya kusikia kilele za ng'ombe na ndipo aliamua Kutoka nje na kuita majirani kwa ajili ya kupata msaada.Walifanikiwa kumuua fisi huyo japo alionekana kuwa mbishi kutoka ndani ya zizi.
Wakazi wa kijiji hicho wanalia kwa kupoteza mifugo yao kila kukicha kwani wanadai eneo lao lina fisi wengi sana.
Na:Esko Donald.
Instagram:esko donald
Facebook:Esko Donald.

Tuesday, 1 August 2017

BOLT AFANANISHWA NA MUHAMMED ALI.

Rais wa Shirikisho la riadha duniani (IAAF), Sebastian Coe amesema kuwa, Usain Bolt ana kipaji na ana ushawishi mkubwa miongoni mwa wanariadha kama, Muhammed Ali alivyokuwa na ushawishi miongoni mwa mabondia.
Mwanariadha huyo raia wa Jamaica Bolt ni bingwa wa mbio fupi ambaye ameshinda medali ya dhabau katika michezo ya olimpiki mara nane anatarajiwa kustaafu baada ya mashindano ya ubingwa mjini London yalioanza siku ya Ijumaa.
Coe alimfananisha Bolt na bondia mashauri duniani, Muhammed Ali.
Source:bongo5
Na:Esko Donald.

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...