Staa wa vichekesho,'Ebitoke',Kinachompata huko Instagram muda huu atakaa asahau.Hii imetokea baada ya kupost hii picha ya Hamisa na kuandika 'Happy Birthday Zari the boss Lady'.Mashabiki wa Zari wamemjia juu na kuanza kummiminia matusi ya kutosha.
Tembelea Instagram muda huu ujionee mwenyewe.
Na:Esko Donald.
Saturday, 23 September 2017
HATA WEWE ZINAKUHUSU:KINACHOMPATA EBITOKE MUDA HUU HAWEZI KUSAHAU.
Friday, 22 September 2017
HATA WEWE ZINAKUHUSU,JIONEE MAAJABU YA LEMMA GUYA GEMEDA.
Bila shaka ni wengi hatumfahamu Lemma Guya Gemeda,huyu ni mchoraji maarafu kutoka nchini Ethiopia.Lemma ana umri wa miaka 90 na amechora zaidi ya picha 10,000 ndani ya miaka zaidi ya sabini ambayo amekuwa akifanya kazi hii.Mzee huyu ni maarafu sana kutokana na picha zake ambazo huzichora kwenye ngozi zilizotoka kwa mbuzi au ng'ombe.
Hata picha hii ya mwanamke unayoiona amechora yeye.Kweli kipaji ni maarifa.
Na:Esko Donald.
HATA WEWE ZINAKUHUSU,TAZAMA MSIMAMO WA VIEWS YOU TUBE KATI YA ZILIPENDWA NA SEDUCE ME.
Leo nimekuletea msimamo wa views huko you tube kati ya hizi ngoma mbili yani Zilipendwa kutoka Wasafi na Seduce me kutoka kwa mkali Ali Kiba.
Na:Esko Donald.
Saturday, 16 September 2017
MAJANGA MAKUBWA YAMKUTA ZITTO KABWE.
Majanga makubwa yamemkuta Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe baada ya nyumba yake iliyopo Kibingo, Kata ya Mwandiga mjini Kigoma kuungua kwa moto.
Akiongea na ITV kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui amethibitisha kuteketea kwa nyumba hiyo zikiwemo mali zilizomo ndani ya nyumba hiyo.
Chanzo:ITV
Na:Esko Donald.
Friday, 15 September 2017
HUYU HAPA ALIYECHUKUA NAFASI YA ZARI.
Ikulu ya Madale ni patashika nguo kuchanika,Sahau kuhusu mrembo Hamisa Mobetto na wengine, kwa sasa ni mshindi wa BBA(Big Brother Africa) mwaka 2013 (The Chase) Dillish Mathews ndio habari ya mjini kwa sasa. Mrembo huyo ambaye ni raia wa nchini Namibia anadaiwa kuuingilia penzi la Zari The Bosslady kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu mzima Diamond Platinum.Mfahamu zaidi mrembo huyo kwa kutazama hizi picha hapa chini.
Na:Esko Donald.
KIMBUNGA IRMA CHASABABISHA VIFO 77.
Habari kutoka nchini Marekani zinasema, hadi sasa kimbunga Irma kilichoipiga nchi ya Marekani na visiwa vya Caribbean kimesababisha vifo vya watu 77 nusu yao wakiwa ni kutoka nchini Marekani.
Miongoni mwa watu waliokufa kutokana na kimbunga Irma ni watu wanne kutoka katika kituo cha kulelea wazee cha Holly Wood kilichoko katika jimbo la Florida, jimbo ambalo lilipigwa vibaya na kimbunga hicho.
Wachunguzi wa masuala ya usalama wakati wa kimbunga wanasema, bila shaka watu hao walikufa baada ya kukosa hewa au kupata joto kali baada ya kituo hicho kukosa huduma ya umeme. Huduma ya umeme ililazimika kukatwa katika maeneo mengi ya jimbo la Florida ili kupisha athari za kimbunga Irma.
Habari zinasema wagonjwa watatu walikutwa wakiwa wamekufa ndani ya kituo hicho cha kulelea wazee na wengine watano walikufa baada ya kufikishwa hospitalini.
Source:tbc
Na:Esko Donald.
Wednesday, 13 September 2017
NYAMA YA NGURUWE HULETA KIFAFA KWA BINADAMU.
Nchini Tanzania nyama ya nguruwe ni maarufu katika maeneo mbali mbali ya starehe na imepewa majina mengi ,kama vile mkuu wa meza, kiti moto na mengineyo mengi.
Hata hivyo utafiti wa kisayansi kutoka chuo kikuu cha kilimo cha sokoine ( SUA), umebaini kuwa walaji wa nyama ya nguruwe wako katika hatari ya kupata magonjwa kama vile kifafa kutokana na mnyoo Tegu uliopo kwenye nyama ya nguruwe.
Na:Esko Donald.
Monday, 11 September 2017
HII NI KUMBUKUMBU NZITO ISIYOSAHAULIKA MAREKANI.
Ni kumbukumbu ya shambulizi la kigaidi lililoua maelfu ya watu nchini Marekani
Shambulizi la kigaidi lililotokea nchini Marekani septembe 11 mwaka 2001.
Ni miaka 16 ya kumbukizi ya tukio la shambulizi la kigaidi lililotokea nchini Marekani septembe 11 mwaka 2001 lililoua watu takribani 3000.
Katika muendelezo wa kutafuta wahusika wa tukio hilo, licha ya kikundi cha Alqaida kuwa mshtumiwa wa kwanza bado Marekani inaituhumu nchi ya Saudi Arabia kufadhili washambuliaji wa tukio hilo.
Marekani imesema serikali ya Saudi Arabia ilifadhili vikundi vya kigaidi kutoka mataifa mawili ya kiarabu ambavyo miaka miwili kabla ya tukio vilikua vikipangana namna ya kufanya shambulio hilo lililotokea kati kati ya minara ya biashara.
Hata hivyo serikali ya Saudi Arabia inaendelea kupinga kuhusika kabisa na mkasa huo.
Source:tbc
Na:Esko Donald.
SABA WAUAWA WA KUPIGWA RISASI.
Watu saba wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Dallas, Texas nchini Marekani na wengine wawili wamejeruhiwa.
Inadaiwa kuwa watu hao kabla ya kupigwa risasi na kuuawa walikuwa wakiangalia mpira katika jumba lifahamikalo kama Plano. Hata hivyo mtuhumiwa aliuawa na polisi wa kwanza ambaye aliwahi kufika katika eneo la tukio.
Bado haijafahamika sababu ya mtu huyo kufanya mauaji hayo.
Wakati huo huo jeshi la polisi mjini humo kupitia kwa ofisa wake, David Tilley, amesema bado wanaangalia suala hili kwa kina zaidi.
Source:bongo5
Na:Esko Donald.
MHE.LOWASSA AMTEMBELEA LISSU HOSPITAL NAIROBI.
Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Edward Lowassa amewasili Nairobi nchini Kenya kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa kupigwa risasi ambaye kwasasa ana patiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan nchini humo.
Na:Esko Donald.
MILLION 100 ZATUMIKA KUOKOA MAISHA YA LISSU.
Wakati habari za shambulio la risasi dhidi ya Tundu Lissu zikihamia kwa viongozi wa kidini, Chadema imeeleza gharama zilizotumika hadi sasa kuokoa maisha yake na kuweka bayana kuwa imemuhamishia dereva wake nje ya mipaka kumuepusha na waliofanya shambulio hilo.
Lissu, mwanasiasa ambaye hana woga wa kuzungumza analoamini, alishambuliwa kwa risasi zipatazo 32 wakati akiwa kwenye gari lake lililoegeshwa nje ya majengo ya nyumba anayoishi akiwa Dodoma wakati wa shughuli za Bunge.
Risasi tano zilimpata mwilini, lakini akaepuka kifo na kwa sasa amelazwa Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, ambako hali yake imeelezwa kuwa nzuri.
Taarifa ilkiyotolewa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana jioni pia imeeleza sababu za kumhamishia Lissu Hospitali ya Aga Khan ya jijini Nairobi, Kenya kutoka Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kushukuru wote waliohusika kuokoa maisha yake.
“Maisha ya Mhe Lissu yalikuwa hatarini sana na palihitajika matibabu maalumu na ya haraka sana kutoka kwa madaktari bingwa,” inasema taarifa hiyo.
Imeongeza kuwa matibabu yake pia yalihitaji vifaa tiba visivyo na shaka yeyote ili kuokoa maisha yake baada ya “kazi na kubwa na ya kupongezwa ya awali iliyofanywa na madaktari wetu kadhaa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma”.
Imeongeza kuwa jana, Lissu alikuwa akifanyiwa upasuaji mwingine.
“Hofu kuu ya usalama wa Mhe Lissu na dereva wake ilitanda kote nchini Tanzania baada ya shambulio dhidi ya uhai wao kushindwa kufanikiwa,” anasema Mbowe katika taarifa hiyo.
“Busara ya kiusalama ilitulazimisha kuwatoa wahanga nje ya mipaka ya nchi hadi hapo usalama wao utakapohakikishwa.
Mbowe anasema shambulio hilo lilimuumiza sana Lissu na ameokoka kimiujiza.
“Kutokana na ukweli huu, matibabu yake vilevile ni maalum na yanayohitaji wataalam wengi, vifaa tiba maalum na gharama kubwa,” anasema.
“Hadi sasa, zaidi ya Sh.100 milioni zimeshatumika kuokoa maisha ya ndugu yetu Lissu.
“Thamani ya Mhe. Lissu, ni kubwa kuliko kiwango chochote cha fedha. Kila njia iliyo halali itatumika kupata fedha za kutosha kumtibu Mhe. Lissu na hatimaye kumrudisha kwenye uwanja wa kudai haki, demokrasia na ustawi kwa wote nchini Tanzania.”
Taarifa hiyo inasema “dereva wa Mhe. Lissu, Simon Mohamed Bakari naye tunaye hapa Nairobi akiendelea kupata huduma za kisaikolojia”.
“Alishuhudia shambulio lile na aliokoka kimiujiza. Anasumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo. Naye hatukuona busara kuendelea kumuacha nchini hadi hapo hali yake ya kiafya na kiusalama itakapohakikishwa,” anasema Mbowe.
“Ni dhahiri kwa aina ya shambulio lilivyokuwa, wauaji walikusudia kuwaua wote; Mhe. Lissu na hata dereva wake.”
Chadema imerejea mazungumzo baina ya Serikali na chama hicho kuhusu hospitali gani apelekwe kutoka Dodoma.
“Upande wangu na Wabunge wetu wa Ukawa ulisisitiza Mhe. Lissu apelekwe moja kwa moja Nairobi na kama Bunge na Serikali hawatakuwa tayari kubeba gharama za kuokoa maisha ya Mhe. Lissu, basi sisi na Watanzania wenye mapenzi mema watachangia gharama hizo za kuokoa maisha kitibabu na kiusalama,” amesema Mbowe.
Mbowe amesema Lissu alitibiwa na madaktari wapatao kumi wa fani tofauti baada ya kufika Nairobi na walifanya kazi hiyo usiku kucha na anaendelea kutibiwa muda wote akiwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu, lakini juzi aliweza kuzungumza.
“Kwa mara ya kwanza, Mhe. Lissu aliongea jana jioni na mkewe Alucia na baadaye na mimi, akisema ‘mwenyeki, I survived to tell the tale (niliokoka ili nisimulie mkasa). tafadhari, endeleeni kupambana”.
Amesema watu kutoka sehemu mbalimbali wamekuwa wakitaka kumtemebelea, lakini hawaruhusiwi na ulinzi umeimarishwa katika eneo analotibiwa.
“Hairuhusiwi wageni kumuona hadi hapo madaktari wakiridhika kuwa hali yake ya kimatibabu inaruhusu,” alisema.
Chadema imeeleza katika taarifa hiyo kuwa Tanzania si Salama, ikirejea mauaji ya mwenyekiti wa chama hicho mkoani Geita, Alphonce Mawazo aliyeuawa mwaka 2015, kamatakamata za wanaharakati na kuteswa kwa kilichoitwa makosa ya kimtandao.
Pia imetaja kutoweka kwa mshauri wa Mbowe, Ben Saanane na kutekwa kwa wasanii na kuteswa; kutaifishwa kwa mali, mashamba na biashara za viongozi wa upinzani.
Source: Mwananchi
Na:Esko Donald
Thursday, 7 September 2017
LISSU APIGWA RISASI MKOANI DODOMA.
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amekimbizwa hospitali mchana huu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mchaa akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa ametoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji.
Kwa upande wa mwanasiasa wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe Ruyagwa amewataka watanzania kuendelea kumuomba mwanasiasa huyo ambaye ni Mbunge wa Singida.
“Tumwombee Tundu Lissu. Kila mtu aombe Kwa imani yake. Mungu ampe nafuu inshallah,” alitweet Zitto.
Source:eatv
Na:Esko Donald.
Saturday, 2 September 2017
TUPO TAYARI KWA RAUNDI YA PILI_KENYATA
Baada ya Mahakama nchini Kenya kupinga matokeo ya urais nchini humo,kupitia ukurasa wake wa Instagram rais Uhuru Kenyatta amesema wanaamini katika demokrasia na wako tayari kwa raundi ya pili ya uchaguzi.Ameongeza na kusema kuwa wanaamini katika amani na umoja wa nchini yao.
Na:Esko Donald.
Friday, 1 September 2017
KOLASINAC ATUA ARSENAL BUREE.
Dirisha la usajili kwa Arsenal lilitawaliwa na wachezaji wanaotoka kuliko wanaoingia. Arsene Wenger amewashuhudia Alex Oxlade-Chamberlain, Kieran Gibbs, Wojciech Szczesny na Gabriel Paulista wakiondoka klabuni hapo, wakati Alexis Sanchez akiendelea kubaki baada ya kushindwa kutimkia Manchester City.
Arsenal walifanikiwa kumsajili Sead Kolasinac, beki wa kushoto kutoka FC Schalke kwa uhamisho huru.
Kolasinac aliingia kwenye kikosi bora cha Bundesliga msimu uliopita ataongeza nguvu kwenye kikosi cha Arsenal na ni mtu mwenye mapafu ya chuma.
Umahiri alioonyesha kwenye mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Chelsea unaashiria kwamba ataifaa klabu ya Arsenal.
Na:Esko Donald.
Source:Goal.com
MAHAKAMA YAFUTA MATOKEO YA URAIS KENYA.
Mahakama yafuta matokeo ya uchaguzi wa urais Kenya.Mahakama ya Juu nchini Kenya imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi uliopita katika uamuzi kuhusu kesi iliwasilishwa na muungano wa upinzani National Super Alliance.
Na:Esko Donald.
JIFUNZE KUPITIA HADITHI.
…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...

-
Linapojatwa jina la Director Nisher bila shaka itakuwa unakumbuka video ya nyimbo ya Young D "Kijukuu" na nyingine nyingi ambazo z...
-
Madrid yafanikiwa kuandika historia mpya baada ya kulichukua kombe hili mara mbili mfululizo.
-
Na:Esko Donald. Esko Wa Simulizi 'EWS'. Jesca binti wa Kimasai mwenye rangi ya bahati kuliko mabinti wote kijijini kwao alikuwa ni...
-
Bila shaka ni wengi hatumfahamu Lemma Guya Gemeda,huyu ni mchoraji maarafu kutoka nchini Ethiopia.Lemma ana umri wa miaka 90 na amechora zai...
-
……JESCA…… Episode ya 2 Na:Esko Donald. Esko Wa Simulizi 'EWS'. Whatsapp:0675730796. Ilipoishia.. BAADA YA MIAKA MITATU. Jesca...