Monday, 24 July 2017

EBITOKE ADAI KUCHANGANYWA NA KISS LA KWANZA KUTOKA KWA BEN POL

Mchekeshaji kutoka Timamu Media, Ebitoke ambaye kwa sasa anadaiwa kuwa mapenzini na Rnb Super Star Bongo, Ben Pol ameelezea moment aliyokutanayo siku ya kwanza muimbaji huyo alipomkiss.
“Unajua mtu unayempenda halafu akikukiss lazima mwili usisimke kwanza, yeah mimi nilisisimka, nilisema mama!!!, nilihisi kama nipo mbinguni,” amesema Ebitoke.
Katika mahojiano na EATV alipoulizwa ex boy friend wake anachukuliaje drama zinazoelndelea kati yake na Ben Pol, mchekesaji huyo aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa hajawahi kuwa na mtu.
“Sina boy friend na sijawahi kudate na mtu, Ben ndio wangu wa kwanza,” alisisitiza.
Source:bongo5
Na:Esko Donald

Thursday, 20 July 2017

BEKA WA YAMOTO BAND AWEKWA CHINI YA ULINZI

Msanii wa Bongo Flava, Beka Flavour anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini katika kituo cha Tabata Dar es Salaam kwa tuhuma za kutapeli kupitia mtandao.
Taarifa za awali kutoka kwa mtu wa karibu wa msanii huyo zinaeleza kuwa Beka ameshikiliwa kuanzia saa tano asubuhi baada ya kijana mmoja kuripoti kutapeliwa katika mtandao wa facebook kupitia jina la msanii huyo.
Jitihada za kumtoa zinaendelea kufanywa na watu wake wa karibu.
Taarifa zaidi Nitakujuza.
Source:Bongo5
Na:Esko Donald.

Tuesday, 18 July 2017

ANUSURIKA KUVUNJWA MKONO NA NG'OMBE.

Kijana mmoja mkoani Tanga aliyefahamika kwa jina la Erick Mallya anusuruka kuvunjwa mkono na Ng'ombe wakati anaendelea na zoezi zima la ukamuaji.Tukio hili limetokea mapema asubuhi ya leo katika chuo cha mifugo kiitwacho LITA_Buhuri.Taarifa zinasema kuwa,wakati kijana huyu anaanza kukamua,ghafla alishuhudia teke zito likirushwa kuelekea maeneo ya mkono wake wa kushoto.Hali hii ilisababisha kijana huyu kujinasua kwa haraka sana kutoka kwa ng'ombe huyo kwa ajili ya Usalama wake.Inasemekana hali hii ilisababishwa na kitendo cha kusahau kuifunga miguu ya nyuma ya ng'ombe huyo.
Na:Esko Donald.
Instagram @esko donald.

Thursday, 13 July 2017

BIFU ZITO KATI YA RAMA DEE NA CLOUDS FM LAFIKA TAMATI.

Baada ya kuchuniana kwa kipindi kirefu, hatamaye msanii wa RnB Bongo, Rama Dee amemaliza tofauti yake na kituo cha radio cha Clouds Fm.
Kupitia kipindi cha XXL Rama Dee alitumia fursa hiyo kuomba radhi kwa yote yaliyotokea kipindi cha nyuma na kueleza kuwa ni muda wa kufanya muziki mzuri.
“Mimi nasema kwa mashabiki wangu wote wa Clouds Fm na kote wanakonisikiliza, sasa hivi ni muda wa sisi kukaa sehemu moja. Kwa hiyo, kwa chochote ambacho kimetokea kwa Rama Dee ambacho kilionekana si sahihi, naweza kusema I m sorry” amesema Rama Dee na kuongeza.
“Na kwa Clouds Fm kwa wao wenyewe wanaona kwamba kuna sehemu walinikosea, tayari tumeshazungumza na tumeshamaliza kwa hiyo tupo sehemu nzuri na bila shaka upendo uendelee,” alimaliza kwa kusema.
Ikumbukwe kuwa Rama Dee ndiye aliyekuwa akifanya chorus katika ngoma za ‘kundi’ la Anti-Virus ambalo lilitoa albamu za kukishambulia kwa maneno kituo hicho cha radio, hata hivyo Rama Dee amesema katika albamu zilizotoka hakuna sehemu aliyotukana.
Source:bongo5
Na:Esko Donald

Tuesday, 11 July 2017

TUKIO LA KUSIKITISHA,AJALI YA NDEGE YAPOTEZA ROHO 16.

Watu 16 wamefariki papo hapo kwenye ajali ya ndege ya jeshi huko Mississipi nchini Marekani.
Ajali hiyo ilitokea katika Kaunti ya LeFlore karibia kilomita 160 kusini mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Jackson.
Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la utangazaji la Reuters Watu wote 16 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia huku chanzo cha ajali kikiwa bado hakijafahamika.
Hata hivyo jarida la kiserikali la jimbo la Mississipi limeandika kuwa ndege hiyo ilianguka katika shamba moja na mabaki yake kutapakaa maeneo tofauti tofauti.
Ndege hiyo yenye namba KC-130 ni moja ya ndege za kijeshi zenye gharama kubwa zinazotumiwa na Jeshi la Marekani, kupitia ukurasa rasmi wa twitter wa Jeshi la Majini wamethibitisha taarifa hizo huku wakieleza kuwa taarifa zaidi zitatolewa kesho kuhusu ajali hiyo.
Source:bongo5
Na:Esko Donald.

Saturday, 8 July 2017

JE WEWE NI MTUMIAJI WA KAHAWA.

Naaam,habari yako mpenzi msomaji.Uuzaji wa kahawa au biashara ya kuuza kahawa imekuwa ikipanda chati kila kukicha.Mkoa wa Tanga umekuwa ni moja kati ya Mikoa ambayo biashara hii inafanyika.Kwa kuthibitisha hili kila ifikapo mishale ya jioni utaona sehemu tofauti tofauti pembezoni mwa barabara kukiwa na meza za kahawa.Wapenzi wakubwa wa kinywaji hiki usema kuwa,ili kufaidi utamu wa kahawa sharti ushushie na kipande cha kashata ambacho huongeza ladha mdomoni mwa mtumiaji.Wengine huongeza kwa kusema kuwa,ili kinywaji hiki kilete ladha zaidi sharti kutawale mazungumzo ya ubishi miongoni mwa watumiaji.
Utafiti umeonyesha kuwa asilimia kubwa ya watumiaji wa kinywaji hiki wa watu wazima tofauti na vijana.
Vipi kuhusu wewe Mdau,mara ya mwisho kutumia Kahawa ilikuwa ni lini?
Na:Esko Donald.

Friday, 7 July 2017

MWANAMKE MWENYE NDEVU NYINGI NA ASIYEJUTIA HALI HIYO.

Kupitia jarida la Guinness,Harnaam Kaur mwenye umri wa miaka 25 ametajwa kuwa ndiye mwanamke mwenye ndevu nyingi zaidi na akiongeza kwa kusema hajutii kufuga ndevu hizo.
Na:Esko Donald.
Instagram @esko donald
Facebook @esko donald.

Saturday, 1 July 2017

PENGINE NISHER ANAKUJA KUWATOA MACHOZI AKINA HANSCANA.

Linapojatwa jina la Director Nisher bila shaka itakuwa unakumbuka video ya nyimbo ya Young D "Kijukuu" na nyingine nyingi ambazo zimefanywa na Director huyu siku za nyuma.Kwa kipindi kirefu Nisher ameonekana kuwa kimya sana huku soko likitekwa na Directors wengine kama vile Hanscana,Kwetu studio,Khalfani na wengine wengi.
Tunaweza kusema kimya kingi kina mshindo,hii ni kutokana na Nisher kuposti picha masaa machache yaliyopita kupitia ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa Location sambamba na Camera zenye thamani kubwa.Pengine huu ndio unaweza kuwa ndio ujio wake mpya,ebu tusubiri tuone.
Na:Esko Donald.
Instagram @esko donald.
Facebook @esko donald.

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...