Friday, 30 June 2017

ELIMU KUBWA YA MWANAMKE HUSABABISHA HILI.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Twaweza, umebaini kuwa uwezo wa akili ya watoto shuleni unategemea sana na kiwango cha elimu cha mama.

Aidha, watoto wenye mama mwenye elimu hufaulu zaidi kuliko wale wenye mama asiye na elimu na ufaulu huongezeka kulingana na kiwango cha elimu cha mama.

Na:Esko Donald.

Thursday, 29 June 2017

DIAMOND HAWA MUUZA KARANGA.

Mkali wa Bongo flavour Diamond Platinum baada ya bidhaa yake ya Chibu Perfume,sasa hivi amekuja na DIAMOND KARANGA.
Kupitia mitandao ya kijamii Diamond ameandika haya,

"Am glad to inform you that today have launched my new Product called @DiamondKaranga (Diamond Peanuts)  which will be available in East Africa for 300/= Tanzanian Shilling retail Price and 20,000/= Wholesale Price .....
(Leo nimezindua Bidhaa yangu mpya iitwayo @Diamondkaranga ambayo itakuwa inapatikana Madukani kote Africa Mashariki nzima kwa shilingi miatatu tu (300/=) bei ya rejareja kwa pakiti moja... na shilingi elf ishirini (20,000) kwa boksi moja  lenye pakiti Mia moja (100)  ndani ambazo ukiuza unapata faida ya elf kumi... Karanga hizi nazinunua kwa wakulima kutoka mikoa ya DODOMA, MTWARA,  TABORA n.k.... kisha kuziongezea njonjo na kuzipakia katika pakiti za kisasa, ili mtu mwenye hadhi yoyote aweze kutembea nazo popote atakapo... ) usiseme tena Karanga sema DIAMOND KARANGA!!!!"
Na:Esko Donald.

Wednesday, 28 June 2017

MFAHAMU RAIS ASIYEKUBALIKA ZAIDI DUNIANI.

Rais Donald Trump wa Marekani ametajwa kama Rais asiyekubalika zaidi kuwahi kuchaguliwa na Taifa hilo takwimu zikionesha zaidi ya 80% ya wananchi hawampendi na zaidi ya 40% ya waliomchagua kujutia uamuzi wao, kwa mujibu wa Taasisi ya utafiti ya Pew Research Center.
Utafiti huo pia umeonesha Rais Trump ameisababishia Marekani kupoteza nguvu na ushawishi duniani ambapo zaidi ya nchi 37 zilizohusishwa kwenye utafiti huo ni nchi mbili pekee Urusi na Israel zilionesha kumkubali Rais huyo.
Sababu kubwa ziliyotajwa Trump kutokubalika ukilinganisha na mtangulizi wake Barack Obama ni sera yake ya kuwafukuza wahamiaji na kujenga ukuta kuitenganisha nchi yake na Mexico.
Aidha, Utafiti umeonesha kuwa Rais mstaafu Obama bado anakubalika kwa 90% katika ardhi ya Korea Kusini na Trump akikubalika kwa 10% huku Israel ikionekana kumkubali zaidi Trump kwa 56% huku Obama akikubalika kwa 49%.
Na:Esko Donald.

Sunday, 25 June 2017

RAIA 123 WATEKETEA KWA MOTO,PAKISTAN.

Watu 123 wamethibitishwa kufa, baada ya lori lililokuwa likibeba mafuta na lililopata ajali ya barabarani kushika moto na kuteketea nchini Pakistan.
Janga hilo limefanyika katika mji wa Ahmedpur Sharqia katika jimbo la Punjap; hayo ni kwa mjibu wa viongozi wa serikali.
Watu wengine kadhaa wameteketea vibaya, pale walipokuwa wakijaribu kuteka mafuta kutoka katika lori hilo la mafuta.
Waliojeruhiwa wanatibiwa hospitali. Wazima moto wamo katika eneo la ajali wakijaribu kukabiliana na moto huo.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zasema kuwa, lori hilo la mafuta lililokuwa likiendeshwa kwa kasi, lilipinduka, kuanguka na kisha kushika moto.
Mashuhuda wanasema kuwa, baadhi ya watu waliofika katika eneo la ajali walikuwa wakivuta sigara, jambo ambalo linakisiwa kuwa chanzo cha moto huo, hiyo ni kwa mjibu wa runinga ya Geo TV ya Pakistan.
Source:Bongo5
Na:Esko Donald.

Saturday, 24 June 2017

BET AWARD MIKONONI MWA RAYVANNY.

Staa wa Bongo Flava, Rayvanny kutoka WCB ameshinda tuzo ya BET kipengele cha Viewers Choice Best New International Act Artist.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram C.E.O wa WCB Diamond Platinum akusita kuandika maneno haya,

"Hatimaye leo Unakuja nayo Tanzania Dah!
….Zaidi ya miaka mi 3 tunaenda na kurudi Patupu….Hakika Maisha Uvumilivu na kutokata tamaa…. BRING IT HOME BOSS!!! @babutale ‘
‘THE BET Viewers Choice Best New International Act 2017 !!!!!!!!!!!!!
WOOOOOOOOOYOOOOOOOO!!!!!!!….. Nikishindwa kwa Mkono wa Kulia, ntatumia hata Mkono wa Kushoto…..ila lazma ifike @Wcb_Wasafi TANZANIA!!!! Chkua hiyo
#Wcb_Wasafi #WinningTeam !".
Na:Esko Donald.

PICHA 9 ZA MUONEKANO WA SASA WA MUIMBAJI WA INJILI,BREATICE MHONE.

Wengi wanamfahamu Breatice Mhone kwa ubora wake wa kuimba nyimbo za kuabudu.Nimekuletea Muonekano wa sasa wa muimbaji huyu wa Injili.
Na:Esko Donald.

HALI YA WASTARA SI SHWARI.

Hali ya kiafya ya muigiza wa Filamu Bongo, Wastara si nzuri kwa sasa ambapo inaelezwa kuwa jana usiku alipoteza fahamu.
Tatizo hilo limemkumba Wastara akiwa nchini Kenya alipokwenda kufanya kazi zake. Taarifa zilitolewa na uongozi wake kupitia ukurasa wa Instagram anaoumiliki yeye mwenyewe umesema hadi sasa hali yake sio nzuri na kuwaomba watanzania kumuombea ili kupona haraka.

"Habari za Asubuhi Wapendwa Naomba Tumuweke kwenye Sala Zetu Dada Yetu mpendwa Wastara, kutokana na hali yake Anasumbuliwa na maumivu ya mgongo ambayo yanampelekeaga kupoteza Fahamu, Jana usiku yamemkuta matatizo hayo akiwa nchini Kenya ambako yupo kikazi.
Amelazwa huko na hali yake bado siyo nzuri . Tunaomba Dua zenu wapendwa iliarudi kwenye hali yake ya kawaida".
#Imetolewanauongozi
Na:Esko Donald.

Wednesday, 21 June 2017

KUKWEPA KODI MWIKO.

Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa serikali itaendelea kubana mianya yote ambayo imekuwa ikitumiwa na baadhi ya Kampuni kujinufaisha na kuifanya Tanzania kuwa maskini.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Kibaha mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku Tatu mkoani humo ambapo pamoja na mambo mengine atazindua viwanda Vitano na kufungua barabara ya Msata - Bagamoyo.
Kuhusu tatizo la umeme mkoani Pwani, Rais Magufuli amesema amemuomba Waziri Mkuu wa Ethiopia kutuma wataalam wake wa nishati ili kuja kusaidia utaalam wa kujenga bwawa kubwa la maji ambalo lilifanyiwa utafiti tangu utawala wa Rais wa Kwanza wa Tanzania.
Rais Magufuli leo ameendelea na ziara yake wilayani Kibaha ambapo pamoja na mambo mengine amezindua ujenzi wa kiwanda cha kuunganishia matrekta kilichopo Tamko.
Source:tbc
Na:Esko Donald.

CHILAMBO AMEKULETEA HII.

Unapolisikia jina la Walter Chilambo nadhani litakuwa si geni masikioni mwako.Tangu alipoamua kuugeukia mziki wa Injili amesababisha watu wengi kumfuatilia na kutaka kujua ni kipi anaweza kufanya ndani ya gospel.Lakushangaza imekuwa tofauti na matazamio ya wengi,asilimia kubwa ya watu walijua pengine aliingia kwenye mziki wa Injili kwa nguvu ya Soda.Kwa kuthibitisha hilo,baada ya kuachia nyimbo yake ya kwanza kwa upande wa gospel iliyofahamika kwa jina la ASANTE,kwa sasa Chilambo kwa spidi ya risasi amekuja na nyimbo yake mpya aliyoipa jina NAMBA 1.
Unaweza kuipata nyimbo hii kupitia Mkito.com.
Na:Esko Donald.
Instagram@Esko Donald.
Facebook@Esko Donald.

Tuesday, 20 June 2017

FAIDA YA MAZOEZI KWA MAMA MJAMZITO.

Naaam,habari yako ndugu msomaji,nadhani wote tunafahamu kuwa katika jamii zetu kumekuwa na utamaduni wa kutokufanya mazoezi hususani akina Mama wajawazito.Mama mjamzito huwa katika hali hii kwa muda wa miezi tisa ambapo anashauriwa kufanya mazoezi kwa kipindi hicho.
Zifuatazo ni baadhi ya faida za kufanya mazoezi kwa Mama mjamzito,
1.Humuongezea nguvu.
2.Husaidia kumpa usingizi mzuri.
3.Humfanya ajisikie vizuri muda wote.
4.Humuandaa kwa ajili ya kujifungua bila matatizo yeyote.
5.Uchochea muonekano mzuri.
6.Baada ya kujifungua, mwili wa Mama ujirudi kwenye hali yake ya awali kwa haraka mno.
7.Upunguza uzito.
8.Uboresha kinga ya mwili.
Na:Esko Donald.
Instagram@Esko Donald.
Facebook@Esko Donald.

SHABIKI DAMU WA YANGA AFARIKI DUNIA.

Kama ni shabiki wa soka la Tanzania hususani Dar es salaam Young Africans wana Jangwani najua utakuwa umfahamu vizuri shabiki maarufu wa Yanga ambaye amekuwa na utamaduni wa kuifuata timu mahali popote inapokwenda (Ally Yanga) .
Taarifa ya kusikitisha  kuhusiana na
Ally Yanga inasema  kuwa amefariki dunia katika ajali ya gari huko mkoani Dodoma eneo la Ipogolo.Ally Yanga imeripotiwa kuwa alikuwa katika mbio za Mwenge.
Na:Esko Donald.
Instagram@Esko Donald
Facebook@Esko Donald

TIOTE AZIKWA MJINI ABIDJAN.

Kiungo wa zamani wa timu ya Newcastle United na timu ya Taifa ya Ivory Coast Cheki Tiote aliefariki dunia nchini China amezikwa kwenye mji wa kibiashara wa Abidjan.
Tiote aliyekuwa akiichezea timu ya Beijing Enterprises alikutwa na mauti wakati akiwa mazoezi.
Maziko hayo yamehuhuriwa na waziri mkuu wa nchi hiyo Amadou Gon Coulibaly, waziri wa michezo Albert Amichia na rais wa shirikisho la soka la nchi hiyo Augustin Sidy Diallo huku baadhi ya nyota wa soka wa nchi hiyo wakiwemo Salomon Kalou pamoja na mshambuliaji anaecheza soka England Wilfred Bony ambapo wachezaji wote waliweza kuelezea masikitiko ya kifo hicho na namna walivyocheza na marehemu katika michezo mbali mbali.
Source:tbc
Na:Esko Donald

Monday, 19 June 2017

SERIKALI YATAJA NCHI UNAZOWEZA KUSAFIRI BILA VISA.

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kuwa zipo nchi 67 ambazo Watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesema hayo leo bungeni alipojibu swali la mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi aliyetaka kufahamu nchi hizo.
Mhandisi Massauni amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo kupitia tiketi ya CCM Rashid Shangazi lililohoji
Tanzania imeridhia mikataba mbalimbali ya Kimataifa ikiwepo Dimplomasia ya mahusiano, Je ni nchi ngapi na zipi ambazo Watanzania wanaweza kutembelea moja kwa moja kwa utaratibu wa Visa on entry wakati wa kuingia ukiondoa nchi za Jumuiya ya Mashariki?
“Visa huambatana na masharti ambayo hutolewa na nchi husika ili kuwarusu raia wa kigeni kuingia au kuondoka nchini kwa muda maalum fursa hiyo inapotolewa katika vituo vya kuingilia nchini inajulikana kama Visa on arrival, utaratibu wa Visa on arrival uko katika sura ya makubaliano au Mikataba baina ya nchi na nchi au taratibu zinazotokana na matengamano na ushirikiano wa Kimataifa kikanda, utaratibu huu unaweza kubadilika kutokana na makubaliano na hali ya usalama kati ya nchi na nchi, Zipo nchi 16 ambazo Watanzania wanaweza kuzitembelea katika utaratibu wa Visa on arrival ya kuwa na viza na duniani zipo 67 Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, GuineaBissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone pamoja na Togo pamoja na utaratibu huu wa Visa on arrival pia zipo nchi 67 duniani Watanzania wanaweza kuzitembelea bila kuhitaji visa,” alisema Mhe. Masauni.
“Ni kweli nchi za Jumuiya Madola zinautaratibu wa kutembeleana wananchi wake bila ya kuwa na visa lakini kama nilivyo jibu katika swali langu la msingi kwamba ushirikiano na matengemano hayo ya jumuiya ya madola utaratibu wake unaweza kubadilika kulingana na mahusiano na hali ya kiusalama ,kwa hiyo siyo jambo la kushangaza kuona India na Nigeria kwamba nchi hizi mbili zipo kwenye Uanachama wa Jumuiya ya Madola lakini utaratibu wa visa kuna ‘level’ unakuwa hautumiki,” alisisitiza Masauni.
Source:bongo5
Na:Esko Donald.

MBWA 347 WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI MANYARA.

Jumla ya Mbwa 347 kati ya zaidi ya 3600 wanaozurura mitaani katika mji wa Babati mkoani Manyara wameuawa kwa kupigwa risasi na Idara ya mifugo ya Halmashauri ya mji wa Babati.
Mbwa hao wameuawa katika kipindi cha mwezi Mei na Juni mwaka huu kufuatia ongezeko kubwa la Mbwa wanaozurula mitaani na kutishia usalama wa Wakazi wa mji wa Babati ambapo katika kipindi cha kuanzia Junuari hadi mwishoni mwa Mei mwaka huu jumla ya watu 264 waling’atwa na Mbwa.
Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya mji wa Babati Dakta Fatuma Mkombozi amesema zoezi hilo ni endelevu mpaka watakapowateketeza mbwa wote wanazurura mitaani na kutishia amani.
Kwa mujibu wa sensa ya mifugo ya mwaka 2016 mji wa Babati unakadiriwa kuwa na Mbwa 4,923 ambao kati yao Mbwa 3,693 sawa na asilimia 75 wanazurula mitaani na asilimia 35 ya wanaozurula mitaani hawana wamiliki.
Source:tbc
Na:Esko Donald.

Sunday, 18 June 2017

SAMATTA ASAINI DILI MUHIMU KWA AJILI YA WATANZANIA.

Nahodha wa Taifa Stars na mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubeligiji, Mbwana Samatta ameingia mkataba maalumu na Benki ya DTB na pia ataendesha kliniki ya soka kwa mamia ya vijana zoezi lililofanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete, Kidongo Chekundu Dar es Salaam.
Akizungumzia mkataba huo, Samatta alisema una lenga la kuhamasisha vijana ili kuendeleza soka la Tanzania.
“Nitakuwa balozi wa DTB (Diamond Trust Bank), nikifanya kazi mbalimbali za kijamii na masuala ya kimichezo,” alisema Samatta muda mfupi baada ya kumaliza kutoa mafunzo ya soka.
Na:Esko Donald.

JE RONALDO ANAWEZA KUBADILI MAWAZO YAKE NA KUENDELEA KUBAKI REAL MADRID.

Mshambuliaji wa timu ya Real Madrid ataka kuondoka kwenye timu hiyo kwenye majira haya ya usajili ya kiangazi hasa baada ya kukumbwa na kashfa ya kutokulipa kodi.
Taarifa zinasema Ronaldo hataki tena kubaki nchini Hispania na amechukizwa mno na kashfa hiyo ambayo mwenyewe anasema hajafanya kosa hilo na amekuwa akilipa kodi wakati wote.
Ronaldo alijiunga na mabingwa hao wa Kihistoria barani Ulaya mwaka 2009 akitokea Manchester United ya England kwa dau la paundi milioni 80 ambayo ilikuwa ni rekodi ya dunia na kwa kipindi chote hicho ameifungia Real Madrid mabao 406 katika michezo 394 na wiki chache zilizopita aliisaidia kuweka rekodi ya Ulaya baada ya kufanikiwa kutetea taji lao la ligi ya mabingwa.
Sasa watu wanajiuliza, je Ronaldo anaweza kubadili mawazo yake na kuendelea kubaki Real Madrid au la na kama ataondoka ataenda wapi na hali itakuwaje Real Madrid bila yeye? Hayo ni maswali ambayo mashabiki wa soka wanajiuliza.
Taarifa zinasema kama Cristiano Ronaldo akiondoka Real Madrid anaweza kutimkia nchini China ambako timu kadha zinamuwinda kwa udi na uvumba lakini pia kuna taarifa zinasema anaweza kwenda kujiunga na PSG ya Ufaransa.
Pamoja na hayo yote Real Madrid imetoa taarifa ikisema hawana wasiwasi na mchezaji huyo kwani wana uhakika atabaki kwenye timu yao na swala hilo la kudaiwa kodi litamalizwa na ukweli utajulikana.
Na:Esko Donald.

25 WAFARIKI KWA MOTO URENO.

Watu 25 wamefariki dunia na wengine takriban 20 wamejeruhiwa kutokana na moto mkubwa uliozuka katika msitu uliopo katikati mwa nchi ya Ureno.
Kwa mujibu wa taarifa ya awali iliyotolewa na serikali ya nchi hiyo imedai, watu wengi walifariki wakati walipokuwa wakijaribu kuyakimbia maeneo ya Pedrogao Grande yaliyopo Kusini Mashariki mwa mji wa Coimbra.
Naye waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, João Gomes amewaambia waandishi habari kuwa watu 16 wameteketea ndani ya magari yao hadi kufa, pale walipokabiliwa na moto huo mkubwa katika Wilaya ya Pedrógão Grande katika barabara inayounganisha miji ya Figueiro dos Vinhos na Castanheira de Pera.
Wakati huo huo waziri mkuu António Luís Santos da Costa, amesema hilo ni tukio baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.
Source:Bongo5
Na:Esko Donald.

MAJERUHI WA LUCKY VICENT KUREJEA NCHINI AGOSTI.

Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha, walionusurika katika ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva huenda wakarejea nchini baada ya miezi miwili.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ametoa taarifa hiyo katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram
Katika MAHOJIANO yao na WANAHABARI MADAKTARI wamesema WATOTO wote watatu Doreen, Sadia na Wilson wanategemewa KUTEMBEA tena, na kwamba HUENDA wakaruhusiwa kurejea TANZANIA baada ya miezi miwili ijayo. MTOTO Doreen anatarajiwa kuhamishiwa Madonna Center, katika mji wa Lincoln, Jimbo la Nebraska kwa “therapy” maalumu ya uti wa Mgongo wiki ijayo. Wamesema katika WOTE watatu, Doreen ni MUUJIZA mkubwa zaidi
Source:Bongo5
Na:Esko Donald

MZEE YUSUPH AFIWA NA MKEWE.

Aliyekuwa Mfalme wa muziki wa Taarabu nchini Tanzania, Alhaj Mzee Yusuf jana usiku amefiwa na mke wake wa pili wa ndoa ajulikanae kwa jina la Chiku Khamis baada ya upasuaji (Operation) uzazi kutokwenda salama.

Mzee Yusuf amesema mke wake alianza kuugua uchungu wa uzazi kuanzia asubuhi jana na alipoona hali yake inazidi kuwa mbaya ndipo alipochukua uamuzi wa kumpeleka Hospitali ya Amana ambako alifanyiwa upasuaji na kwa bahati mbaya mtoto akazaliwa akiwa ameshafariki na muda mfupi baadae mama mzazi nae akaaga Dunia.
Source:Bongo5
Na:Esko Donald.

Friday, 16 June 2017

FILAMU YA ALL EYES ON ME YA TUPAC YATOKA RASMI.

Filamu ya ‘All Eyes On Me’ iliyotengenezwa kwa ajili ya kuonesha maisha halisi ya marehemu Tupac Shakur imetoka rasmi.
‘All Eyes On Me’ iliyozinduliwa juzi na hatimaye siku ya Jana kupitia kituo cha runinga cha HBO ikaanza kuruka, Filamu hiyo ilianza kutengenezwa tangu mwaka jana katika miji mbali mbali ikiwemo Altanta, Sin City na mingineyo nchini Marekani huku ikiwa chini ya mtayarishaji, L.T. Hutton.
Kijana aitwaye Demetrius Shipp Jr. ameigiza katika filamu hiyo kama Tupac huku Danai Gurir akiigiza nafasi ya Afeni Shakur ambaye ni mama mzazi wa rapper huyo ambaye alifariki mwezi Mei, mwaka jana.
Siku ya kuachiwa filamu ya maisha ya Tupac yatajwa rasmi
Tupac alipigwa risasi baada ya kutoka katika pambano la ndondi kati ya Mike Tyson na Bruce Seldon, Septemba 7, 1996. Na alifariki dunia Septemba 23 mwaka huo baada ya kupoteza damu nyingi.
Source:Bongo 5
Na:Esko Donald

Thursday, 15 June 2017

WAFUKUZWA KAZI BAADA YA KUUOZESHA MKONO WA KICHANGA.

Wauguzi wawili wa Hospitali ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida wamesimamishwa kazi baada ya kumuacha mtoto wa miezi minne na kamba ya kufungia dripu mkononi kwa masaa 4 hali iliyopelekea mkono wa kushoto wa mtoto huyo kuoza na huenda akakatwa vidole au mkono huo.
Kitaalamu hali hii ya kuoza kwa mkono imesababishwa na kukosekana oxygen ya kutosha katika eneo ambalo juu yake kulikuwa na kamba hiyo.Oxygen hufika maeneo mbali mbali mwilini kwa kusafirishwa kupitia kwenye damu.Kitendo cha kumuacha na kamba ya kufungia dripu ilipelekea kukosekana damu ya kutosha katika eneo husika,kitaalamu kitendo hiki kinaitwa Ischemia.

Na:Esko Donald.

Monday, 12 June 2017

RONALDO APATA WATOTO MAPACHA.

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amepata watoto wawili mapacha kutoka kwa mpenzi wake wa siri.
Taarifa kutoka kwenye kituo cha runinga cha SIC zimeeleza kuwa watoto hao mapacha walizaliwa Alhamisi ya wiki iliyopita na majina ya watoto hao ni Mateo na Eva .
Licha ya taarifa hizo kuzagaa, Ronaldo bado ameendelea kuliweka jambo hilo kuwa siri kama ilivyo kuwa kwa mtoto wake wa kwanza, Ronaldo Jr.
Kwasasa Ronaldo yupo na mpenzi wake mwanamitindo wa Kihispania aitwaye, Georgina Rodriguez ambaye hivi karibuni ilielezwa kuwa ni mjamzito.
Source:bongo 5
Na:Esko Donald.

PROF.MAGHEMBE AYASIKITIKIA MAISHA YA WAHADZABE.

Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amesikitishwa na hali duni ya maisha ya jamii ya Wahadzabe, Watindiga na Watatoga wanaoishi katika Bonde la Yaeda Chini Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara.
Prof Maghembe amesema haiwezekani jamii hiyo ikaendelea kuishi kwa kula Unga wa Mibuyu, Mizizi na Wanyamapori wakati kila siku watalii wanaenda katika bonde hilo kuangalia jamii hiyo.
Katika risala yao iliyosomwa na Daines Naftari mwanajamii ya Wahadzabe wamesema Majangili wamesababisha kutoweka kwa Wanyamapori wanaowatumia kama kitoweo chao na ukame ukitajwa kusababisha njaa.
Source:tbc
Na:Esko Donald.

Sunday, 11 June 2017

MAN U WALETA KOMBORA JIPYA LA ULINZI.

Manchester United wameafikia makubaliano ya kumsaini mlinzi raia wa Sweden Victor Lindelof kutoka Benfica kwa kima cha pauni milioni 31.

United wanasema kuwa kilichobakia ni makubaliano ya kibinafsi na uchunguzi wa kiafya ambavyo viitafanyika wiki ijayo.

Lindelof, ambaye ameichezea nchi yake mara 12 anatarajiwa kushiriki mechi ya kirafiki nchini Norway siku ya Jumanne

Mchezaji huyo mwenye maiak 22 ambaye amekuwa akiichezea Benfica tangu mwaka 2012 atakuwa mchezaji wa kwanza kusainiwa na Man U msimu huu.

Lindelof alicheza mara 47 klabu hiyo ya Ureno msimu uliopita.
Na:Esko Donald.

WAPOTEZA MAISHA BAADA YA MAPIGANO YA KUGOMBEA CHAKULA NCHINI SOMALIA.

Zaidi ya watu 14 wamekufa na wengine kumi wamejeruhiwa nchini Somalia wengi wao wakiwa ni raia baada ya kuzuka mapigano baina ya wanajeshi wakigombea chakula cha misaada.
Habari zinasema mapigano hayo  yametokea katika Mji wa Baidoa ambao una maelfu ya raia wanaohitaji misaada ya chakula kutokana na kukabiliwa na ukame na uhaba mkubwa wa chakula.
Mapigano hayo yalizuka baada ya baadhi ya wanajeshi kujaribu kuiba chakula cha misaada ambapo kundi jingine la wanajeshi lilikuja na kuwazuia.
Maafisa wa hospitali Mjini Baidoa wamesema baadhi ya majeruhi hao wana hali mbaya na wanaendelea kupata matibabu.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa Somalia inakabiliwa na ukame na hivyo kuiongezea matatizo nchi hiyo ya Pembe ya Afrika inayokabiliwa pia na tatizo la njaa na ukosefu wa amani na usalama.
Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, nusu ya raia wa Somalia ambao ni karibu watu Milioni sita na laki mbili wanahitajia msaada wa haraka huku watoto Laki Tatu Na Elfu 63 wakikabiliwa na hali mbaya ya utapiamlo.
Na:Esko Donald.

FAHAMU FAIDA ZA MAFUTA YA NAZI MWILINI.

Mafuta ya nazi ni matuta ambayo hutokana na nazi, na hapa utengenezwa kwa kukuna nazi, kisha kukamua tui zito na baadae kulipika tui hilo hadi kugeuka kuwa mafuta.
1. Husaidia afya ya Moyo
Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa ajili afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla.
2. Huongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
Mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo wa mwili kukimeng’enya chakula, watu wanaoyatumia mafuta haya kupikia vyakula vyao kila siku kwa kawaida huwa na uzito wa kawaida. Anasema Geeta Sidhu Robb, mtaalamu wa lishe na mwanzilishi wa Nosh Detox.
3. Huongeza nguvu mwilini
Ni chanzo kizuri cha nguvu mwili kwani yana sifa ya kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu ‘medium chain triglycerides – MCT’ ambapo susafiri moja kwa moja hadi kwenye ini na hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu au hubadililishwa kuwa ‘ketones’.
4. Mubadala ya kupikia
Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, pia ni mazuri kwa wasiopenda mafuta ya wanyama. Kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto, hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!
5. Hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu
Mafuta ya nazi yanao uwezo kuziamusha seli za ubongo na katika kusaidia kuzuia matatizo ya uwendawazimu au ukichaa (dementia) na kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
6. Husaidia katika ugonjwa wa aleji
Moja wapo ya faida ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji, kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.
Zingatia :
Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100, Ila ni vizuri kuyatengeneza mwenyewe ilikuepuka kuchanganyiwa na kemikali nyingine na kama unapikia kwenye chakula chenye nazi kama wali usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.
Source:Bongo 5
Na:Esko Donald.

Sunday, 4 June 2017

50 WAPOTEZA MAISHA MOSUL,IRAQ

Duru za habari kutoka mji ulioharibiwa wa Mosul nchini Iraq, zinasema kuwa raia kadhaa wameuwawa, pale walipokuwa wakiukimbia mji huo, kunusuru maisha yao, dhidi ya mapigano mabaya yanayotekelezwa na wanamgambo wa Islamic State.

Wanahabari wa runinga ya Reuters, wamepata maiti ya wanaume, wanawake na watoto, zikiwa zimetapakaa katika barabara za mji huo.

Hilo limetukia katika Wilaya ya Zanjili, karibu na eneo la mapigano, ambapo jeshi la taifa ya Iraq, linakabiliana vikali na wanamgambo hao wa Dayesh, kama wanavyofahamika.

Mfanyikazi mmoja wa shirika la utoaji misaada la Marekani- Dave Eubank, amesema kuwa wapiganaji wa I-S, wamekuwa wakiwamiminia risasi wananchi wanaojaribu kuutoroka mji huo.

Anasema kuwa ameona maiti 50, lakini kwa msaada wa jeshi la Marekani linalosaidiana na wanajeshi wa Iraq, amefaulu kuwaokoa watu wawili tu.
Source:BBC Swahili.
Na:Esko Donald.

Saturday, 3 June 2017

PICHA ZA MABINGWA WA CHAMPIONS LEAGUE 2016/2017,REAL MADRID.

Madrid yafanikiwa kuandika historia mpya baada ya kulichukua kombe hili mara mbili mfululizo.

PICHA YA BECKHAM NA BINTI YAKE,SERENGETI YAZUA UTATA HADI KWAO.

Jina la staa wa soka wa zamani wa kimataifa wa England David Beckham limezidi kuchukua headlines baada ya wiki hii kuonekana akiwa Tanzania katika hifadhi ya Serengeti akiwa pamoja na familia yake watoto wake wanne na mkewe Victoria wakila bata.

Ilijulikana kuwa Beckham yupo Tanzania baada ya kusambaa kwa video fupi akionekana Beckham na familia yake Airport Dar es Salaam,
Beckham amepiga picha kadhaa na kuzipost instagram akiwa Serengeti lakini picha na mtoto wake wa mwisho Harper imekuwa topic.
Picha aliyopiga David Beckham akimkiss mtoto wake Harper Seven katika lips baadhi ya mashabiki wanaomfollow wameonekana kuikosoa na kuona haipo katika maadili na wengine wakiona haina shida, mjadala ambao umeendelea hadi mtandao wa mirror.co.uk wa
England ambapo ndio kwao na David Beckham.
Na:Esko Donald.

REAL MADRID YAFANYA KUFURU.

Klabu ya Real Madrid ya nchini Uhispania imeichakaza Juventus ya Italia 4-1 na kushinda Kombe la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya huku ikiweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kuchukua ubingwa mara mbili mfululizo.
Mreno Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili, la kwanza kwake na klabu dakika ya 20 na lake la pili dakika ya 64.
Casemiro aliwafungia Real bao lao la pili dakika ya 61 kabla ya Asensio kukamilisha ushindi wao dakika ya 90 kwa bao lao la nne.
Juventus, waliokuwa wameanza vyema mechi hiyo wakikuwa wamekomboa bao la kwanza la Ronaldo dakika ya 27 kupitia Mario Mandzukic na kufanya mambo kuwa sare wakati wa mapumziko lakini kipindi cha pili mawimbi yaliwageuka.
Nguvu mpya wao Juan Cuadrado alipewa kadi ya pili ya manjano dakika ya 84, baada ya kukaa uwanjani dakika 18 pekee.
Gareth Bale aliingia kwenye mechi hiyo kama nguvu mpya, mara yake ya kwanza kuchezeshwa mechi ya ushindani tangu 23 Aprili.
Mechi hiyo iliyochezewa Cardiff ilikuwa ya 19 kwa klabu hizo mbili kukutana, mechi zote zikiwa katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya.
Klabu hizo ndizo zilizokutana mara nyingi kabisa historia ya michuano hiyo, baada ya Bayern dhidi ya Real Madrid (24).
Na:Esko Donald.

"JAZA UJAZWE" YALETA UTATA BUNGENI.

Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku anayejulikana kwa jina la Msukuma, ametaka Tangazo la Tigo la Jaza Ujazwe lisitishwe kwa kuwa linaleta maana mbaya kwa kiswahili na tamaduni za kitanzania
Naibu Spika Tulia Ackson amesema TCRA ndio wanahusika na hilo na watachukua hatua stahiki kama itatakiwa
Amewataka pia wabunge kuwa makini kwa kuwa kuna matangazo mengine ni feki yenye lengo la kuharibu sifa za kampuni kwa sababu za kibiashara
Na:Esko Donald.

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...