Wednesday, 2 August 2017

SHAMBULIZI LA FISI KIJIJINI BALANG'DALALU.

Mkulima mmoja mkoani Manyara katika Wilaya ya Hanang,kijiji cha Balang'dalalu avamiwa na fisi kwenye zizi lake la ng'ombe usiku wa kuamkia leo,mishale ya saa nane usiku.
Fisi huyo alifanikiwa kumjeruhi vibaya ng'ombe mmoja kwa kumng'ata maeneo ya mdomoni kuelekea eneo la juu ya uso.
Mkulima huyo alisema kuwa,alishtuka baada ya kusikia kilele za ng'ombe na ndipo aliamua Kutoka nje na kuita majirani kwa ajili ya kupata msaada.Walifanikiwa kumuua fisi huyo japo alionekana kuwa mbishi kutoka ndani ya zizi.
Wakazi wa kijiji hicho wanalia kwa kupoteza mifugo yao kila kukicha kwani wanadai eneo lao lina fisi wengi sana.
Na:Esko Donald.
Instagram:esko donald
Facebook:Esko Donald.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...