Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya, ambao ulishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, umeapa kuendelea na maandamano wenye nia ya kubatilisha kile ambacho unasema kuwa, matokeo "feki" ya uchaguzi mkuu.
Mpinzani mkuu wa Bw Kenyatta, Bw Raila Odinga, amedai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na wizi mkubwa wa kura.
Upinzani Kenya wadai Odinga ndiye mshindi wa urais.
Seneta James Orengo ameiambia BBC kuwa chama chake, kinachoongozwa na Bw Raila Odinga, hakitapinga matokeo ya uchaguzi mkuu mahakamani, huku akisema kuwa Uhuru Kenyatta tayari ametoa vitisho kwa majaji.
Kufikia sasa watu 11 wameuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu, ambazo zilianza mara tu baada ya Uhuru Kenyatta kushinda kutangazwa mshindi kwa muhula wa pili mnamo usiku wa kuamkia Jumamosi.
Tume ya taifa ya kutetea haki za kibinadamu nchini Kenya, imetoa orodha ya juu ya wahasiriwa wa ghasia hizo huku ikisema kuwa ni watu 24 ndio ambao wameuwawa katika visa vinavyohusiwa na uchaguzi huo, huku ikiongeza kuwa polisi wanatumia nguvu kupita kiasi.
Kaimu Waziri wa usalama wa ndani, Fred Matiangi, amewataja waandamanaji kama "wahalifu".
Source:bbcswahili.
Na:Esko Donald.
Sunday, 13 August 2017
VURUGU ZAUWA WATU NCHINI KENYA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
JIFUNZE KUPITIA HADITHI.
…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...

-
Linapojatwa jina la Director Nisher bila shaka itakuwa unakumbuka video ya nyimbo ya Young D "Kijukuu" na nyingine nyingi ambazo z...
-
Madrid yafanikiwa kuandika historia mpya baada ya kulichukua kombe hili mara mbili mfululizo.
-
Na:Esko Donald. Esko Wa Simulizi 'EWS'. Jesca binti wa Kimasai mwenye rangi ya bahati kuliko mabinti wote kijijini kwao alikuwa ni...
-
Bila shaka ni wengi hatumfahamu Lemma Guya Gemeda,huyu ni mchoraji maarafu kutoka nchini Ethiopia.Lemma ana umri wa miaka 90 na amechora zai...
-
……JESCA…… Episode ya 2 Na:Esko Donald. Esko Wa Simulizi 'EWS'. Whatsapp:0675730796. Ilipoishia.. BAADA YA MIAKA MITATU. Jesca...
No comments:
Post a Comment