Monday, 11 September 2017

SABA WAUAWA WA KUPIGWA RISASI.

Watu saba wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Dallas, Texas nchini Marekani na wengine wawili wamejeruhiwa.
Inadaiwa kuwa watu hao kabla ya kupigwa risasi na kuuawa walikuwa wakiangalia mpira katika jumba lifahamikalo kama Plano. Hata hivyo mtuhumiwa aliuawa na polisi wa kwanza ambaye aliwahi kufika katika eneo la tukio.
Bado haijafahamika sababu ya mtu huyo kufanya mauaji hayo.
Wakati huo huo jeshi la polisi mjini humo kupitia kwa ofisa wake, David Tilley, amesema bado wanaangalia suala hili kwa kina zaidi.
Source:bongo5
Na:Esko Donald.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...