Thursday, 15 June 2017

WAFUKUZWA KAZI BAADA YA KUUOZESHA MKONO WA KICHANGA.

Wauguzi wawili wa Hospitali ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida wamesimamishwa kazi baada ya kumuacha mtoto wa miezi minne na kamba ya kufungia dripu mkononi kwa masaa 4 hali iliyopelekea mkono wa kushoto wa mtoto huyo kuoza na huenda akakatwa vidole au mkono huo.
Kitaalamu hali hii ya kuoza kwa mkono imesababishwa na kukosekana oxygen ya kutosha katika eneo ambalo juu yake kulikuwa na kamba hiyo.Oxygen hufika maeneo mbali mbali mwilini kwa kusafirishwa kupitia kwenye damu.Kitendo cha kumuacha na kamba ya kufungia dripu ilipelekea kukosekana damu ya kutosha katika eneo husika,kitaalamu kitendo hiki kinaitwa Ischemia.

Na:Esko Donald.

2 comments:

  1. Duuu pole kwa mwenye mtoto,,,, polen wauguzi pia maana nadhan n bahat mbaya tu
    Hakuna apenday kuumiz kwa kusudi pasipo sabb

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mungu wa mbinguni akuponye mtoto akufanyie wepesi pale palipo pagumu,,,,, Amen

      Delete

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...