Friday, 16 June 2017

FILAMU YA ALL EYES ON ME YA TUPAC YATOKA RASMI.

Filamu ya ‘All Eyes On Me’ iliyotengenezwa kwa ajili ya kuonesha maisha halisi ya marehemu Tupac Shakur imetoka rasmi.
‘All Eyes On Me’ iliyozinduliwa juzi na hatimaye siku ya Jana kupitia kituo cha runinga cha HBO ikaanza kuruka, Filamu hiyo ilianza kutengenezwa tangu mwaka jana katika miji mbali mbali ikiwemo Altanta, Sin City na mingineyo nchini Marekani huku ikiwa chini ya mtayarishaji, L.T. Hutton.
Kijana aitwaye Demetrius Shipp Jr. ameigiza katika filamu hiyo kama Tupac huku Danai Gurir akiigiza nafasi ya Afeni Shakur ambaye ni mama mzazi wa rapper huyo ambaye alifariki mwezi Mei, mwaka jana.
Siku ya kuachiwa filamu ya maisha ya Tupac yatajwa rasmi
Tupac alipigwa risasi baada ya kutoka katika pambano la ndondi kati ya Mike Tyson na Bruce Seldon, Septemba 7, 1996. Na alifariki dunia Septemba 23 mwaka huo baada ya kupoteza damu nyingi.
Source:Bongo 5
Na:Esko Donald

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...