Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kuwa zipo nchi 67 ambazo Watanzania wanaweza kusafiri bila ya kuwa na viza.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesema hayo leo bungeni alipojibu swali la mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi aliyetaka kufahamu nchi hizo.
Mhandisi Massauni amebainisha hayo leo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo kupitia tiketi ya CCM Rashid Shangazi lililohoji
Tanzania imeridhia mikataba mbalimbali ya Kimataifa ikiwepo Dimplomasia ya mahusiano, Je ni nchi ngapi na zipi ambazo Watanzania wanaweza kutembelea moja kwa moja kwa utaratibu wa Visa on entry wakati wa kuingia ukiondoa nchi za Jumuiya ya Mashariki?
“Visa huambatana na masharti ambayo hutolewa na nchi husika ili kuwarusu raia wa kigeni kuingia au kuondoka nchini kwa muda maalum fursa hiyo inapotolewa katika vituo vya kuingilia nchini inajulikana kama Visa on arrival, utaratibu wa Visa on arrival uko katika sura ya makubaliano au Mikataba baina ya nchi na nchi au taratibu zinazotokana na matengamano na ushirikiano wa Kimataifa kikanda, utaratibu huu unaweza kubadilika kutokana na makubaliano na hali ya usalama kati ya nchi na nchi, Zipo nchi 16 ambazo Watanzania wanaweza kuzitembelea katika utaratibu wa Visa on arrival ya kuwa na viza na duniani zipo 67 Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, GuineaBissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone pamoja na Togo pamoja na utaratibu huu wa Visa on arrival pia zipo nchi 67 duniani Watanzania wanaweza kuzitembelea bila kuhitaji visa,” alisema Mhe. Masauni.
“Ni kweli nchi za Jumuiya Madola zinautaratibu wa kutembeleana wananchi wake bila ya kuwa na visa lakini kama nilivyo jibu katika swali langu la msingi kwamba ushirikiano na matengemano hayo ya jumuiya ya madola utaratibu wake unaweza kubadilika kulingana na mahusiano na hali ya kiusalama ,kwa hiyo siyo jambo la kushangaza kuona India na Nigeria kwamba nchi hizi mbili zipo kwenye Uanachama wa Jumuiya ya Madola lakini utaratibu wa visa kuna ‘level’ unakuwa hautumiki,” alisisitiza Masauni.
Source:bongo5
Na:Esko Donald.
Monday, 19 June 2017
SERIKALI YATAJA NCHI UNAZOWEZA KUSAFIRI BILA VISA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
JIFUNZE KUPITIA HADITHI.
…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...

-
Linapojatwa jina la Director Nisher bila shaka itakuwa unakumbuka video ya nyimbo ya Young D "Kijukuu" na nyingine nyingi ambazo z...
-
Madrid yafanikiwa kuandika historia mpya baada ya kulichukua kombe hili mara mbili mfululizo.
-
Na:Esko Donald. Esko Wa Simulizi 'EWS'. Jesca binti wa Kimasai mwenye rangi ya bahati kuliko mabinti wote kijijini kwao alikuwa ni...
-
Bila shaka ni wengi hatumfahamu Lemma Guya Gemeda,huyu ni mchoraji maarafu kutoka nchini Ethiopia.Lemma ana umri wa miaka 90 na amechora zai...
-
……JESCA…… Episode ya 2 Na:Esko Donald. Esko Wa Simulizi 'EWS'. Whatsapp:0675730796. Ilipoishia.. BAADA YA MIAKA MITATU. Jesca...
No comments:
Post a Comment