Jumla ya Mbwa 347 kati ya zaidi ya 3600 wanaozurura mitaani katika mji wa Babati mkoani Manyara wameuawa kwa kupigwa risasi na Idara ya mifugo ya Halmashauri ya mji wa Babati.
Mbwa hao wameuawa katika kipindi cha mwezi Mei na Juni mwaka huu kufuatia ongezeko kubwa la Mbwa wanaozurula mitaani na kutishia usalama wa Wakazi wa mji wa Babati ambapo katika kipindi cha kuanzia Junuari hadi mwishoni mwa Mei mwaka huu jumla ya watu 264 waling’atwa na Mbwa.
Daktari wa Mifugo wa Halmashauri ya mji wa Babati Dakta Fatuma Mkombozi amesema zoezi hilo ni endelevu mpaka watakapowateketeza mbwa wote wanazurura mitaani na kutishia amani.
Kwa mujibu wa sensa ya mifugo ya mwaka 2016 mji wa Babati unakadiriwa kuwa na Mbwa 4,923 ambao kati yao Mbwa 3,693 sawa na asilimia 75 wanazurula mitaani na asilimia 35 ya wanaozurula mitaani hawana wamiliki.
Source:tbc
Na:Esko Donald.
Monday, 19 June 2017
MBWA 347 WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI MANYARA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
JIFUNZE KUPITIA HADITHI.
…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...

-
Linapojatwa jina la Director Nisher bila shaka itakuwa unakumbuka video ya nyimbo ya Young D "Kijukuu" na nyingine nyingi ambazo z...
-
Madrid yafanikiwa kuandika historia mpya baada ya kulichukua kombe hili mara mbili mfululizo.
-
Na:Esko Donald. Esko Wa Simulizi 'EWS'. Jesca binti wa Kimasai mwenye rangi ya bahati kuliko mabinti wote kijijini kwao alikuwa ni...
-
Bila shaka ni wengi hatumfahamu Lemma Guya Gemeda,huyu ni mchoraji maarafu kutoka nchini Ethiopia.Lemma ana umri wa miaka 90 na amechora zai...
-
……JESCA…… Episode ya 2 Na:Esko Donald. Esko Wa Simulizi 'EWS'. Whatsapp:0675730796. Ilipoishia.. BAADA YA MIAKA MITATU. Jesca...
No comments:
Post a Comment