Tuesday, 20 June 2017

TIOTE AZIKWA MJINI ABIDJAN.

Kiungo wa zamani wa timu ya Newcastle United na timu ya Taifa ya Ivory Coast Cheki Tiote aliefariki dunia nchini China amezikwa kwenye mji wa kibiashara wa Abidjan.
Tiote aliyekuwa akiichezea timu ya Beijing Enterprises alikutwa na mauti wakati akiwa mazoezi.
Maziko hayo yamehuhuriwa na waziri mkuu wa nchi hiyo Amadou Gon Coulibaly, waziri wa michezo Albert Amichia na rais wa shirikisho la soka la nchi hiyo Augustin Sidy Diallo huku baadhi ya nyota wa soka wa nchi hiyo wakiwemo Salomon Kalou pamoja na mshambuliaji anaecheza soka England Wilfred Bony ambapo wachezaji wote waliweza kuelezea masikitiko ya kifo hicho na namna walivyocheza na marehemu katika michezo mbali mbali.
Source:tbc
Na:Esko Donald

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...