Sunday, 18 June 2017

MAJERUHI WA LUCKY VICENT KUREJEA NCHINI AGOSTI.

Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha, walionusurika katika ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva huenda wakarejea nchini baada ya miezi miwili.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ametoa taarifa hiyo katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram
Katika MAHOJIANO yao na WANAHABARI MADAKTARI wamesema WATOTO wote watatu Doreen, Sadia na Wilson wanategemewa KUTEMBEA tena, na kwamba HUENDA wakaruhusiwa kurejea TANZANIA baada ya miezi miwili ijayo. MTOTO Doreen anatarajiwa kuhamishiwa Madonna Center, katika mji wa Lincoln, Jimbo la Nebraska kwa “therapy” maalumu ya uti wa Mgongo wiki ijayo. Wamesema katika WOTE watatu, Doreen ni MUUJIZA mkubwa zaidi
Source:Bongo5
Na:Esko Donald

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...