Friday, 1 September 2017

KOLASINAC ATUA ARSENAL BUREE.

Dirisha la usajili kwa Arsenal lilitawaliwa na wachezaji wanaotoka kuliko wanaoingia. Arsene Wenger amewashuhudia Alex Oxlade-Chamberlain, Kieran Gibbs, Wojciech Szczesny na Gabriel Paulista wakiondoka klabuni hapo, wakati Alexis Sanchez akiendelea kubaki baada ya kushindwa kutimkia Manchester City.
Arsenal walifanikiwa kumsajili Sead Kolasinac, beki wa kushoto kutoka FC Schalke kwa uhamisho huru.
Kolasinac aliingia kwenye kikosi bora cha Bundesliga msimu uliopita ataongeza nguvu kwenye kikosi cha Arsenal na ni mtu mwenye mapafu ya chuma.
Umahiri alioonyesha kwenye mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Chelsea unaashiria kwamba ataifaa klabu ya Arsenal.
Na:Esko Donald.
Source:Goal.com

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...