Friday, 15 September 2017

KIMBUNGA IRMA CHASABABISHA VIFO 77.

Habari kutoka nchini Marekani zinasema, hadi sasa kimbunga Irma kilichoipiga nchi ya Marekani na visiwa vya Caribbean kimesababisha vifo vya watu 77 nusu yao wakiwa ni kutoka nchini Marekani.
Miongoni mwa watu waliokufa kutokana na kimbunga Irma ni watu wanne kutoka katika kituo cha kulelea wazee cha Holly Wood kilichoko katika jimbo la Florida, jimbo ambalo lilipigwa vibaya na kimbunga hicho.
Wachunguzi wa masuala ya usalama wakati wa kimbunga wanasema, bila shaka watu hao walikufa baada ya kukosa hewa au kupata joto kali baada ya kituo hicho kukosa huduma ya umeme. Huduma ya umeme ililazimika kukatwa katika maeneo mengi ya jimbo la Florida ili kupisha athari za kimbunga Irma.
Habari zinasema wagonjwa watatu walikutwa wakiwa wamekufa ndani ya kituo hicho cha kulelea wazee na wengine watano walikufa baada ya kufikishwa hospitalini.
Source:tbc
Na:Esko Donald.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...