Saturday, 8 July 2017

JE WEWE NI MTUMIAJI WA KAHAWA.

Naaam,habari yako mpenzi msomaji.Uuzaji wa kahawa au biashara ya kuuza kahawa imekuwa ikipanda chati kila kukicha.Mkoa wa Tanga umekuwa ni moja kati ya Mikoa ambayo biashara hii inafanyika.Kwa kuthibitisha hili kila ifikapo mishale ya jioni utaona sehemu tofauti tofauti pembezoni mwa barabara kukiwa na meza za kahawa.Wapenzi wakubwa wa kinywaji hiki usema kuwa,ili kufaidi utamu wa kahawa sharti ushushie na kipande cha kashata ambacho huongeza ladha mdomoni mwa mtumiaji.Wengine huongeza kwa kusema kuwa,ili kinywaji hiki kilete ladha zaidi sharti kutawale mazungumzo ya ubishi miongoni mwa watumiaji.
Utafiti umeonyesha kuwa asilimia kubwa ya watumiaji wa kinywaji hiki wa watu wazima tofauti na vijana.
Vipi kuhusu wewe Mdau,mara ya mwisho kutumia Kahawa ilikuwa ni lini?
Na:Esko Donald.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...