Tuesday, 11 July 2017

TUKIO LA KUSIKITISHA,AJALI YA NDEGE YAPOTEZA ROHO 16.

Watu 16 wamefariki papo hapo kwenye ajali ya ndege ya jeshi huko Mississipi nchini Marekani.
Ajali hiyo ilitokea katika Kaunti ya LeFlore karibia kilomita 160 kusini mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Jackson.
Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la utangazaji la Reuters Watu wote 16 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia huku chanzo cha ajali kikiwa bado hakijafahamika.
Hata hivyo jarida la kiserikali la jimbo la Mississipi limeandika kuwa ndege hiyo ilianguka katika shamba moja na mabaki yake kutapakaa maeneo tofauti tofauti.
Ndege hiyo yenye namba KC-130 ni moja ya ndege za kijeshi zenye gharama kubwa zinazotumiwa na Jeshi la Marekani, kupitia ukurasa rasmi wa twitter wa Jeshi la Majini wamethibitisha taarifa hizo huku wakieleza kuwa taarifa zaidi zitatolewa kesho kuhusu ajali hiyo.
Source:bongo5
Na:Esko Donald.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...