Wednesday, 21 June 2017

KUKWEPA KODI MWIKO.

Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa serikali itaendelea kubana mianya yote ambayo imekuwa ikitumiwa na baadhi ya Kampuni kujinufaisha na kuifanya Tanzania kuwa maskini.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Kibaha mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku Tatu mkoani humo ambapo pamoja na mambo mengine atazindua viwanda Vitano na kufungua barabara ya Msata - Bagamoyo.
Kuhusu tatizo la umeme mkoani Pwani, Rais Magufuli amesema amemuomba Waziri Mkuu wa Ethiopia kutuma wataalam wake wa nishati ili kuja kusaidia utaalam wa kujenga bwawa kubwa la maji ambalo lilifanyiwa utafiti tangu utawala wa Rais wa Kwanza wa Tanzania.
Rais Magufuli leo ameendelea na ziara yake wilayani Kibaha ambapo pamoja na mambo mengine amezindua ujenzi wa kiwanda cha kuunganishia matrekta kilichopo Tamko.
Source:tbc
Na:Esko Donald.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...