Saturday, 24 June 2017

HALI YA WASTARA SI SHWARI.

Hali ya kiafya ya muigiza wa Filamu Bongo, Wastara si nzuri kwa sasa ambapo inaelezwa kuwa jana usiku alipoteza fahamu.
Tatizo hilo limemkumba Wastara akiwa nchini Kenya alipokwenda kufanya kazi zake. Taarifa zilitolewa na uongozi wake kupitia ukurasa wa Instagram anaoumiliki yeye mwenyewe umesema hadi sasa hali yake sio nzuri na kuwaomba watanzania kumuombea ili kupona haraka.

"Habari za Asubuhi Wapendwa Naomba Tumuweke kwenye Sala Zetu Dada Yetu mpendwa Wastara, kutokana na hali yake Anasumbuliwa na maumivu ya mgongo ambayo yanampelekeaga kupoteza Fahamu, Jana usiku yamemkuta matatizo hayo akiwa nchini Kenya ambako yupo kikazi.
Amelazwa huko na hali yake bado siyo nzuri . Tunaomba Dua zenu wapendwa iliarudi kwenye hali yake ya kawaida".
#Imetolewanauongozi
Na:Esko Donald.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...