Sunday, 18 June 2017

JE RONALDO ANAWEZA KUBADILI MAWAZO YAKE NA KUENDELEA KUBAKI REAL MADRID.

Mshambuliaji wa timu ya Real Madrid ataka kuondoka kwenye timu hiyo kwenye majira haya ya usajili ya kiangazi hasa baada ya kukumbwa na kashfa ya kutokulipa kodi.
Taarifa zinasema Ronaldo hataki tena kubaki nchini Hispania na amechukizwa mno na kashfa hiyo ambayo mwenyewe anasema hajafanya kosa hilo na amekuwa akilipa kodi wakati wote.
Ronaldo alijiunga na mabingwa hao wa Kihistoria barani Ulaya mwaka 2009 akitokea Manchester United ya England kwa dau la paundi milioni 80 ambayo ilikuwa ni rekodi ya dunia na kwa kipindi chote hicho ameifungia Real Madrid mabao 406 katika michezo 394 na wiki chache zilizopita aliisaidia kuweka rekodi ya Ulaya baada ya kufanikiwa kutetea taji lao la ligi ya mabingwa.
Sasa watu wanajiuliza, je Ronaldo anaweza kubadili mawazo yake na kuendelea kubaki Real Madrid au la na kama ataondoka ataenda wapi na hali itakuwaje Real Madrid bila yeye? Hayo ni maswali ambayo mashabiki wa soka wanajiuliza.
Taarifa zinasema kama Cristiano Ronaldo akiondoka Real Madrid anaweza kutimkia nchini China ambako timu kadha zinamuwinda kwa udi na uvumba lakini pia kuna taarifa zinasema anaweza kwenda kujiunga na PSG ya Ufaransa.
Pamoja na hayo yote Real Madrid imetoa taarifa ikisema hawana wasiwasi na mchezaji huyo kwani wana uhakika atabaki kwenye timu yao na swala hilo la kudaiwa kodi litamalizwa na ukweli utajulikana.
Na:Esko Donald.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...