Monday, 9 October 2017

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA……
Episode ya 3
Na:Esko Donald
Esko Wa Simulizi 'EWS'
Whatsapp:0675730796

Ilipoishia…
Mganga mfawidhi wa Zahanati hiyo aliamua iwe siri ili kulinda kibarua chake kisije kuota nyasi.Cha ajabu zaidi siku ambayo Soyeti alikuwa akifanya ubabazi kwa mama Jesca kumbe kulikuwapo nesi ambaye alibahatika kushuhudia tukio zima kupitia dirisha la nyuma la chumba hicho japokuwa Soyeti alijiridhisha kuwa hakukuwa na mtu mahali pale,alifeli.Nesi hiyo aliyefahamika kwa jina la Nasra hakuwa radhi kusema kwa kuhofia usalama wake.

Endelea nayo...
Hakuna mwanakijiji yoyote aliyefahamu haya.Wengi waliamini tatizo la kisukari ndilo lililopelekea umauti kwa mama Jesca.Inafahamika kuwa baada ya kifo kutokea mwili wa mama Jesca ulirejeshwa nyumbani kwa ajili ya taratibu za mazishi.Ulifikishwa nyumbani mnamo majira ya saa sita mchana.Vilio vya simanzi vilisikika kila kona,kila mtu alikuwa akisikitika ki vyake.Wengi waliumia kwa sababu marehemu aliishi vizuri na kila mtu kijijini hapo.
Taratibu za mazishi zilikamilika,kilichobaki alikuwa anasubiriwa Jesca afike ndio mazishi yafanyike.Usiku ulifika huku ndugu na jamaa wakiendelea kupeana faraja kwa kile kilichotokea kwamba ni kazi ya Mungu haina makosa.Muda wa kulala ulifika,ndipo mwili wa marehemu ukaingizwa ndani ya chumba ambacho ndicho walikuwepo baba Jesca na wadogo zake Jesca(Oropi na Songoi).Chini ya Sakafu kulionekana godoro aina Vita raha ambalo ndilo lilitumika kwa ajili ya kuwalaza baba Jesca na watoto wake.
Ilikuwa ni majira ya saa tisa usiku,kila mmoja alionekana kupitiwa na usingizi.
"Hakikisha unakamilisha kazi niliyokupa sawa".
"Nimekuelewa boss ondoa Shaka".
Haya yalikuwa ni mazungumzo kati ya Soyeti na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Ole.Inaonekana kuna kazi ambayo Ole alitakiwa kuifanya usiku ule.
Kwa mwendo wa kunyatanyata,kijana Ole alikuwa anaelekea kwenye chumba ambacho walikuwepo baba Jesca na familia yake.Mlango wa chumba ulikuwa wazi hivyo ilikuwa ni raisi kwa mtu yoyote kuingia ndani.Ole alifanikiwa kuingia chumbani bila mtu yoyote kumuona.Bila shaka alikuwa anakwenda kukamilisha kazi aliyoambiwa aikamilishe.Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo kwenye usingizi mzito unaweza kusema hawataamka tena,kila mmoja alikuwa anakoroma mithili ya mlevi aliyekunywa pombe aina ya gongo.Hata waliokuwepo wamelala nje walikuwa hawajitambui.Ole akaona huu ndio muda mzuri wa kukamilisha kazi yake kwa sababu watu wote walikuwa fofofo.
ITAENDELEA....... USIKOSE.
JE NI KAZI GANI OLE ALITUMWA KUIFANYA USIKU ULE?
MAJIBU YAPO KWENYE EPISODE YA 4.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...