Sunday, 11 June 2017

WAPOTEZA MAISHA BAADA YA MAPIGANO YA KUGOMBEA CHAKULA NCHINI SOMALIA.

Zaidi ya watu 14 wamekufa na wengine kumi wamejeruhiwa nchini Somalia wengi wao wakiwa ni raia baada ya kuzuka mapigano baina ya wanajeshi wakigombea chakula cha misaada.
Habari zinasema mapigano hayo  yametokea katika Mji wa Baidoa ambao una maelfu ya raia wanaohitaji misaada ya chakula kutokana na kukabiliwa na ukame na uhaba mkubwa wa chakula.
Mapigano hayo yalizuka baada ya baadhi ya wanajeshi kujaribu kuiba chakula cha misaada ambapo kundi jingine la wanajeshi lilikuja na kuwazuia.
Maafisa wa hospitali Mjini Baidoa wamesema baadhi ya majeruhi hao wana hali mbaya na wanaendelea kupata matibabu.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa Somalia inakabiliwa na ukame na hivyo kuiongezea matatizo nchi hiyo ya Pembe ya Afrika inayokabiliwa pia na tatizo la njaa na ukosefu wa amani na usalama.
Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, nusu ya raia wa Somalia ambao ni karibu watu Milioni sita na laki mbili wanahitajia msaada wa haraka huku watoto Laki Tatu Na Elfu 63 wakikabiliwa na hali mbaya ya utapiamlo.
Na:Esko Donald.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

…JESCA…… Episode 4 Na:Esko Donald Esko Wa Simulizi 'EWS' Whatsapp:0675730796 Ilipoishia… Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo ...