…JESCA……
Episode 4
Na:Esko Donald
Esko Wa Simulizi 'EWS'
Whatsapp:0675730796
Ilipoishia…
Kwa muda huo watu wote walikuwa wapo kwenye usingizi mzito unaweza kusema hawataamka tena,kila mmoja alikuwa anakoroma mithili ya mlevi aliyekunywa pombe aina ya gongo.Hata waliokuwepo wamelala nje walikuwa hawajitambui.Ole akaona huu ndio muda mzuri wa kukamilisha kazi yake kwa sababu watu wote walikuwa fofofo.
Endelea nayo…
Ole alijisogeza hadi kwenye Jeneza lililokuwa limeuhifadhi mwili wa mama Jesca.Alilifungua na kuitazama sura ya marehemu,kisha akalifunika Jeneza hilo.Aligeuza shigo yake na kuwatazama baba Jesca na watoto wake.Ole aliamua kutazama juu huku machozi yakimtoka.
Akajikuta anazungumza nafsini,,
"Nimeweka agano na Soyeti,lazima nifanikishe hili".
"Lakini mbona hawana hatia!!! ".
"Ila Soyeti ameniahidi mtonyo wa kutosha".
"Lakini nafsi inaniuma kuyafanya haya".
"Hakuna namna ngoja niifanye kazi nisepe fasta".
Basi baada ya kujiuliza hayo,aliamua kuushika mmoja kati ya Mishumaa iliyokuwa pembezoni mwa Jeneza.Kila mshumaa aliokuwepo pale ambao ulikuwa unawaka,ulikuwa umewekewa kisaani maalumu ili hata kama ikatokea umeisha usilete madhara yoyote ya moto.Baada ya kuwa ameushikilia mshumaa ule kwa kutumia mkono wake wa kushoto huku akiwa anatetemeka aliamua kuudondosha juu ya godoro na kisha kuondoka kwa haraka isiyo kifani.Moto ulianza kusambaa pole pole huku moshi mzito ukianza kusambaa chumbani humo.Tukio lile lilifanya baba Jesca na familia yake kushtuka kwa haraka baada ya moto kufika karibu na miili yao na kuanza kuwaunguza.Wote watatu walikimbilia mlangoni kwa lengo la kutoka nje ili kuyaokoa maisha yao.Katika hali isiyokuwa ya kawaida mlango ulionekana kufungwa wakati hapo awali ulikuwa wazi.Kumbe baada ya Ole kumaliza kufanya kazi yake aliamua kutoka na kuufunga mlango wa chumba hicho kwa nje.Kibaya zaidi moto ulizidi kusambaa kwa kasi ya ajabu huku moshi mzito ukizidi kurindima chumbani humo.
Walijikuta wanashindwa kupiga makelele kwa lengo la kuomba msaada kwa sababu ya wingi wa moshi.Kila mmoja alionekana kupumua kwa tabu hivyo ilikuwa ngumu kupaza sauti.Kwa sasa moto ulikuwa umesambaa chumba kizima.Baba Jesca na watoto wake walianza kupata mateso ya kushambuliwa na moto mwilini.Waliungua vibaya sana.Jeneza la marehemu lilionekana kuwaka moto kwa kasi sana.Ghafla kichwa cha marehemu kilipasuka na kutoa mlio mithili ya gurudumu la gari lililopata pancha.
ITAENDELEA USIKOSE.....