Monday, 9 October 2017

JIFUNZE KUPITIA HADITHI.

……JESCA……
Episode ya 2
Na:Esko Donald.
Esko Wa Simulizi 'EWS'.
Whatsapp:0675730796.

Ilipoishia..
BAADA YA MIAKA MITATU.
Jesca anapokea simu na kuambiwa kifo cha wazazi wake pamoja na wadogo zake ni njama iliyofanywa na mtu wake wa karibu ambaye ni mpenzi wake,mvulana ambaye walipendana sana.Anaambiwa kuwa mpenzi wake ndiye amepelekea maafa haya kutokea.

Tuendelee Nayo.
Taarifa hizi zinakuwa mpya kwa Jesca na pia ilikuwa ngumu kuamini,ni kwa vipi mpenzi wake ndio chanzo cha haya yote,?,hilo lilikuwa swali lililokosa majibu fasaha.Jesca na mpenzi wake walitokea kijiji kimoja japo mpenzi wake familia yake ilikuwa na uwezo wa kifedha kijijini hapo kwa kumiliki mashamba baadhi.Inafahamika kilichomuuwa mama yake Jesca ni tatizo la kisukari na sio zaidi ya hapo,na pia inafahamika kuwa baba yake na wadogo zake Jesca walitekea kwa moto uliotokea bahati mbaya huku chanzo kikisemekana kuwa ni mshumaa uliodondokea juu ya godoro.
SIKU MBILI KABLA YA KIFO CHA MAMA JESCA.
Akiwa kwenye Zahanati ya kijiji,presha ya kupanda inaonekana kumuandama mama Jesca.Matatibu wanaonekana kutumia juhudi ya ziada kuipunguza presha hiyo kwa kumuwekea dripu za dawa.Baada ya muda kupita anakuja mpenzi wake na Jesca kwa lengo la kumjulia hali mama mkwe wake.Alifika na kumkuta akiwa amepitiwa na usingizi mzito.Mpenzi wake na Jesca alikuwa anaitwa Soyeti.Ndani ya chumba hicho hakukuwa na mtu mwengine zaidi ya Soyeti na Mama Jesca.Ghafla Soyeti alionekana kutupa macho huku na kule kutazama kama kuna mtu anakuja,baada ya kuona hali ni shwari,alizamisha mkono wake mfukoni na kutoa bomba la sindano ambalo ndani yake lilionekana kuwa na dawa.Aliamua kuichangana dawa hiyo kwa kuiingiza kwenye dripu ambalo lilikuwa na dawa ya kushusha presha.Ni wazi lengo la Soyeti lilikuwa ni kumuua mama Jesca kwani dawa aliyoitumia ilikuwa ni dawa ya kuogeshea ng'ombe kwa ajili ya kuua kupe inayofahamika kwa jina la Paranex.
Baada ya kufanikisha lengo lake,kwa haraka isiyo  mashaka anaamua kuondoka.Hali ya mama Jesca inabadilika ghafla na kupoteza maisha papo hapo.Baada ya kifo hicho kutokea uchunguzi ulifanyika na kufahamika kuwa mama Jesca aliuawa kwa sumu ila haikufahamika ni nani halihusika.Mganga mfawidhi wa Zahanati hiyo aliamua iwe siri ili kulinda kibarua chake kisije kuota nyasi.Cha ajabu zaidi siku ambayo Soyeti alikuwa akifanya ubabazi kwa mama Jesca kumbe kulikuwapo nesi ambaye alibahatika kushuhudia tukio zima kupitia dirisha la nyuma la chumba hicho japokuwa Soyeti alijiridhisha kuwa hakukuwa na mtu mahali pale,alifeli.Nesi hiyo aliyefahamika kwa jina la Nasra hakuwa radhi kusema kwa kuhofia usalama wake.
ITAENDELEA......... USIKOSE.

No comments:

Post a Comment