Kinara wa muungano upinzani nchini Kenya Raila Odinga, amewashauri wafuasi wake kususia kazi siku ya Jumatatu kama njia ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumanne iliyopita.
Akihutubia wafuasi wake mtaani Kibera, Nairobi kwa mara ya kwanza kabisa tangu kutangazwa matokeo, ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi, Bw Odinga amedai kuwa serikali ilikuwa imepanga kuwaua wafuasi wa upinzani kabla ya kutangazwa matokeo.
Source:bbcswahili.
Na:Esko Donald.
No comments:
Post a Comment