Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amepata watoto wawili mapacha kutoka kwa mpenzi wake wa siri.
Taarifa kutoka kwenye kituo cha runinga cha SIC zimeeleza kuwa watoto hao mapacha walizaliwa Alhamisi ya wiki iliyopita na majina ya watoto hao ni Mateo na Eva .
Licha ya taarifa hizo kuzagaa, Ronaldo bado ameendelea kuliweka jambo hilo kuwa siri kama ilivyo kuwa kwa mtoto wake wa kwanza, Ronaldo Jr.
Kwasasa Ronaldo yupo na mpenzi wake mwanamitindo wa Kihispania aitwaye, Georgina Rodriguez ambaye hivi karibuni ilielezwa kuwa ni mjamzito.
Source:bongo 5
Na:Esko Donald.
No comments:
Post a Comment